ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 1, 2020

RC HAPI APOKEA MSAADA KUTOKA KWA QWIHAYA KUSAIDIA KUPAMBANA NA CORONA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akikabidhiwa msaada wa kusiadia kujikinga na virusi vya corona na mkurugenzi wa kampuni hiyo Leonard Mahenda vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.
Moja ya vitu vilivyotolewa na mkurugenzi wa kampuni hiyo Leonard Mahenda kwa ajili ya kusaidia kupambana na maambukizi ya Corona mkoani Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Kampuni ya uzalizaji wa nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprises imekabidhi msaada wa zaidi ya shilingi milioni kumi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa kwa ajili kuwakinga wananchi na maambukizi ya virusi vya Corona.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa kampuni hiyo Leonard Mahenda alisema kuwa msaada huo unalengo la kuwasaidia wananchi kujikinga na virusi vya Corona ambavyo vimekuwa tishio kwa maisha ya binadamu.

Mahenda alisema kuwa baada ya janga la Corona kampuni hiyo imewiwa na kuweza kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi sh. Milioni 10.

Alivitaja vitu vilivyotolewa na kampuni hiyo kuwa ni simtank 62 zenye ujazo wa lita 250,vitakasa mikono Garoni 15 za Lita tano tano, mavazi maalum kwa ajili ya matabibu 20, sabuni za maji aroni 20 za Lita tano tano thermometer scanner na lengo la msaada ni kuweza kusaidia wananchi na wauguzi waweze kutuhudumia kwa usalama zaidi.

Mahenda alisema kuwa wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa namna ambavyo wanapambana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuwa vimereta taharuki kubwa hapa nchi na dunia nzima.

"Mimi nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa elimu na kupambana na virusi vya Corona kwa lengo la kuokoa maisha ya wa Tanzania " alisema

Awali akipokea msaa huo mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi Alisema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupambana na maambukizi ya virus vya corona mkoani hapa na kuwashakuru kwa kuweza kuvitoa kwa wakati mwafaka ambapo dunia inapambana kuweza kutokomeza virusi hivyo.

Alisema kuwa katika kupambana na virusi hivyo wananchi wanatakiwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu na kuwataka ofisi za serikali zote mkoani hapa kuvaa barakao, kunawa mikono na vitakasa mkono na kutowahudumia wananchi ambao hawajavaa barakao hadi wavae.

Alisema kuwa kila taasisi, na ofisi za watu binafsi wazingatie maagizo ya serikali kwa kuweka vifaa vya usafi na sehemu za starehe kuwe na utaratibu maalum kwa wateja wao na kuacha kuwa na mikusanyiko usiyo na maana.

Aidha Hapi aliwataka watendaji kuwafatilia walimu na wazazi ambao wameanzisha masomo kwa watoto majumbani na kufanya mikusanyiko iliyokatazwa na serikali na Latra na vyombo vya ulinzi na usalama kusimamia uvaaji wa barakao na unawaji wa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka katika vyombo vya usafiri, mabaa na hoteli Lakini pia mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alizipogeza Kampuni ya Asas, Kampuni ya Qwihaya, Sai Energy na Taasisi ya Cliton Foundation ambao wametoa misaada ya Barakoa, dawa na vifaa tiba,nguo maalum za madaktari na waaguzi. Sabuni za maji, tanki za kunawia , themoscanner na vitakasa mikono

No comments: