Advertisements

Sunday, January 17, 2021

Tanzia: Msanii ‘C Pwaa’ Afariki Dunia

MSANII wa Bongo Fleva, Ilunga Khalifa maarufu C Pwaa amefariki Dunia alfajiri ya leo akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ndugu wa karibu wa C Pwaa amethibitisha kuwa Pwaa alikuwa anaugua Pneumonia na alifikishwa Hospitali kwa matibabu, hali yake haikuwa njema hadi umauti unamkuta.

Enzi za uhai wake C Pwaa alifanya vizuri akiwa na kundi la Park Lane pamoja na Suma Lee ambapo walitoa ngoma kama Nafasi Nyingine na Aisha, na baadaye alitoa ngoma zake nje ya kundi zikiwemo Action, Problem, So Pwaa, Six in the Morning nk.

GPL

No comments: