Advertisements

Sunday, April 18, 2021

MISA YA KUMUAGA MPENDWA WETU PETER KIHULA ILIYOFANYIKA NEW YORK CITY

Padri Peter Mushi wa kanisa Katoliki la Mtakatifu Cesilia la New York akiongoza ibada ya misa ya kuaga mwili wa mpendwa wetu Peter Kihula iliyofanyika siku ya Jumamosi April 17, 2021 jijini humo.
Mwakilishi wa Ubalozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York, Kanali George Itang'are akitoa neno kuwafariji wafiwa kwa niaba ya Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York Mhe. Prof. Kennedy Gastorn katika ibada ya kuaga mwili wa mpendwa wetu Peter Kihula iliyofanyika siku ya Jumamosi April 17, 2021.
Shemeji wa marehemu akitoa shukrani na kutoa wasifu wa marehemu.
Familia ya marehemu.
Mmoja ya wanafamilia akitoa neno la shukurani.
WaTanzania wa New York na majirani zao wakijumuika pamoja kumuaga mpendwa wao Peter Kihula katika ibada maalum ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika siku ya Jumamosi April 17, 2021 jijini New York.
Ibada ya kuaga mwili wa mpendwa Peter Kihula ikiendelea.
WaTanzania na majirani zao wakifuatilia Ibada ya kuaga mwili wa mpendwa wao Peter Kihula.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: