Advertisements

Wednesday, April 14, 2021

PROF. KABUDI AKABIDHI OFISI KWA BALOZI MULAMULA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akimkabidhi nyaraka kama ishara ya kukabidhi ofisi kwa kwa Waziri mpya wa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Naibu Waziri Mhe Amour Nassor Amour (Mb) ,Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Palamagamba John Kabudi ambapo diplomasia ya siasa a kimkakati ikiwemo diplomasia ya uchumi vikitajwa kama kipaumbele.

Akizungumza wakati akikabidhi nyaraka na Ilani ya Chama Cha mapinduzi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Palamagamba John Kabudi amesema majukumu na muongozo wa utendaji kazi wa Wizara umetajwa katika ilani ya chama ikiwa ni pamoja na kuifanya sauti ya Tanzania kusikika katika medani za kimataifa sanjari na kuijenga haiba na taswira ya Tanzania katika jumuiya za kimataifa……..INSERT Prof. Palamagamba John Kabudi Waziri wa Katiba na Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amemshukuru mtangulizi wake huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili alichohudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuweka misingi imara ya mahusiano na mataifa mengine dunianiikiwa ni pamoja na kusimamia kikamilifu mikataba yenye tija kwa Taifa na makampuni au mataifa mengine……Balozi Liberata Mulamula,Waziri wa Mambo ya Nje

Tukio hilo la kukabidhiana Ofisi limefanyika katika ofisi za Wizara zilizopo katika mji wa Magufuli Mtumba Jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk,Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katika Tukio jingine aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekabidhiana ofisi na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Dkt Mwigulu Lameck Nchemba ambaye sasa ni Waziri wa Fedha na Mipango na Prof Palamagamba John Kabudi ambaye sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria kwa pamoja wameahidiana ushirikiano katika kutekeleza majukumu katika wizara walizopangiwa lengo kubwa likiwa ni kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kufikia matarajio aliyojiwekea kwa manufaa ya Taifa na Watanzania kwa ujumla

No comments: