ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 29, 2021

WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZA LA MAHABUSU MPANDA WALILIA JAJI

Makatibu Wakuu Profesa Sifuni Mchome ( Katiba na Sheria), Dkt Laurian Ndumbalo (Utumishi) na Dkt, John Jingu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana jambo na viongozi wa Magereza Mkoa wa Katavi mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo yao na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Mpanda ambako wafungwa na mahabusu pamoja na mambo mengine wameomba Mkoa huo upatiwe Jaji

· Waomba Makatibu Wakuu kutumia vikao vyao na Mhe. Rais kuwaombea Jaji

· Waomba matukio ya watuhumiwa kuachiwa na kukamatwa tena yatupiwe jicho

· Walalamikia ubambikiziwaji kesi

Na Mwandishi Maalum

KATAVI-MPANDA


Wafungwa na Mahabusu wa Gereza Mahabusu Mpanda Mkoani Katavi, wamelalamikia kitendo cha mtuhumiwa kukamatwa tena mara tu anapoachiwa na mahakama na kufunguliwa upya mashtaka na upelezi kuanza tena

Wamesema matukio hayo ni ubinyaji wa mnyororo mzima wa utoaji Hakijinai kwa wakati.

Wafungwa na Mahabusu hao wameyasema hayo mwishoni mwa mbele ya Makatibu Wakuu, Sifuni Mchome , Laurian Ndumbalo na John Jingu ambao kwa pamoja walitembelea Gereza Mahabusu Mpanda na kuzungumza na Maafisa, Askari pamoja na Wafungwa na Mahabasu kwa lengo la kujifunza mafanikio na changamoto katika chombo hicho cha utoaji wa Hakijinai.

“ Waheshimiwa Makatibu Wakuu, sisi wafungwa na mahabusu wa Gereza Mahabusu Mpanda, tunatumia nafasi hi kuwaeleza kuwa tatizo la upatikanaji haki kwa wakati limekuwa sugu katika Mkoa wetu wa Katavi. Na jambo la kusikitisha ni kwamba, mtuhumiwa anakaa Gerezani zaidi ya miaka mitatu hadi mine, anapofikishwa mahakamani kesi hiyo inafutwa, lakini hapo hapo mtuhumiwa anakamtwa tena na kesi inaanza upya kana kwamba ndiyo kwanza amekamtwa” akasema msoma risala Paulo Ulaya na kushangiliwa na wafungwa na mahabusu wenzie.

Katika risala yao kwa Makatibu wakuu hao na mbele ya Mkuu wa Magerea Mkoa wa Katavi ACP Wilson Rugamba na Mkuu wa Gereza hilo, SP Moses Mbesela na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzuga, wafungwa na mahabusu hao, wakasema

“ Huu ni uonevu kwa kuwa mtuhumiwa anakuwa amekaa miaka mingi na kuteseka gerezani. Tena cha kusikitisha hata upelelezi unaanza upya na kuchukua muda mrefu sana wakati upelelezi wa kwanza ulishakamilika”

Wafungwa na mahabusu hao walitoa mifano ya kesi nne ambazo zilifutwa na watuhumiwa kukamatwa tena, na hivyo wakawaomba Viongozi hao wasaidie katika eneo hili. Na kukomeza uonevu huo unaofanywa na Jeshi la Polisi kuwatesa wananchi wananchi.

Kuhusu ucheleweshaji wa usikilizwaji wa mashauri yao, wafungwa na mahabusu wa Gereza hilo, wameelezea shauku yao ya kuta awepo Jaji wa Mkoa wa Katavi.

“Sisi wafungwa na mahabusu tunayoheshima kubwa kuwaeleza shauku yetu kuwa tuna tamani na sisi kuletewa Jaji katika Mkoa wetu wa Katavi yaani kuwepo kwa Mahakama Kuu Katavi kutokana na kwamba idadi kubwa ya mahabusu katika gereza hili ni kesi za mauaji ambazo hatima yake inamuhitaji Jaji” wakatoa rai wafungwa hao

Vile vile wamesikitikia kitendo cha kesi za muda mrefu kutopewa kipaumbele katika vikao na wakatoa mfano wa kesi nne ambazo ni za muda mrefu na bado hazijapewa kipaumbele cha kusikilizwa. Na wakaomba wasaidiwe kulisemea jambo hili katika vikao na Mhe. Rais ili basi na wao wa Mkoa wa Katavi wapatiwe Jaji ili pia isaidie kupunguza msongamano .

Kwa sasa kesi zote za mauaji zinasikilizwa Mkaoni Rukwa ambapo inabidi mahabusu wasafirishwe kutoka Mkoani Katavi jambo ambalo kwa Mujibu wa Mkuu wa Gereza hilo SP Moses Mbesela si salama lakini wakati mwingine mahabusu wanashindwa kupelekwa Rukwa kwa ukosefu wa Usafiri ambao ungeweza kuwachukua mahabusu wengi kwa wakati mmoja.

Robo tatu ya mahabusu katika Gereza hilo wanakabiliwa na kesi za mauaji,

Aidha Wafungwa na mahabusu hao wameitaja changamoto nyingine inayobinya myororo wa utoaji haki katika Mkoa wa Katavi ni pamoja na tatizo la kumbakikiziwa kesi.

“Tunaomba tutumie pia nafasi hii kuwaeleleza kuwa katika Mkoa wetu tumekuwa na tatizo la polisi kuwabambikizia kesi wananchi wenu, hivyo tunaomba Mhe. Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria uunde tume yako ichunguze kwa undani kuhusu suala hili na ndio maana utagundua kesi nyingi upepelezi wake haukamiliki kwa wakati kutokana na mazingira ya uundaji wa kesi hewa” wakalalamika wafungwa na mahabusu hao.

Vile vile mahabusu na wafungwa hao wamelalamikia kitendo cha Mahabusu kutoka Mahakama ya wilaya ya Mlele kutopelekwa mahakamani kwa wakati na kwamba wanaomba wasaidie kutokomeza uonvu huo ili na wao wapate kujua hatima ya kesi zao.

Aidha wafungwa na mahabusu hao wameomba Makatibu Wakuu hao kuwasaidia kutokomeza uonevu wa unaofanywa na Polisi wa kushikilia mali za watuhumiwa kwa madai ya kuwa ni vielelezo.

Walitaja pia mifano ya kesi nne ambazo watuhumiwa mali zao zinashikiliwa na polisi, mali ambazo wanasema nyingine zingeweza kusaidia familia zao wakati wao wakiendelea kusubiri hatima yao.

Gereza Mahabusu Mpanda lilianzishwa mwaka 1947, likiwa na uwezo wa kuhifadhi wahalifu 100. Lakini kwa sasa lina jumla ya wahalifu 333 na wakati mwingine wanafika hadi 400.

Pamoja na idadi hiyo kubwa ya mahabusu na wafungwa, Gereza Mkoa wa Katavi lina watumishi 59 ambapo Maafisa ni wanne, na askari wa cheo cha Rank and file ni 55 na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 21 kwa mchanganuo wa Maafisa 6 na askari wa kawaida 15 kwaajiili kukabiliana na shughuli ya ulinzi wa wafungwa na mahabusu.

No comments: