Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Mkutano kati ya mawazi
wa Kenya na Tanzania unaendelea Jijini Arusha ambapo miongoni mwa Agenda kuu ni
kujadili na kutatua vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru.
Mkutano huo ni sehemu
ya utekelezaji wa maazimio ya yaliyofikiwa na wakuu wa nchi za Tanzania na Kenya
wakati wa ziara ya kiserikali ya Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021
Waziri wa Kilimo Mhe
Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo Jijini Arusha tarehe 29 Mei 2021 wakati
akizungumza na kituo cha matangazo cha Azam Tv.
Amesema kuwa katika ziara ya Rais Mhe Samia nchini Kenya pamoja na mambo mengine wakuu hao wan chi waliwahakikishia wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuwa serikali za nchi zote mbili zipo tayari kuwapa ushirikiano wowote watakaouhitaji na kuweka mazingira mazuri ya kukuza biashara na uwekezaji katika nchi zote mbili.
Kwa mujibu wa Waziri Mkenda katika mahojiano hayo na Azam Tv amesema kuwa Mahitaji ya mahindi nchini Kenya ni takribani Tani Laki 6 hivyo vikwazo vilivyopo katika mipaka ya Holili na Namanga havina tija kwa nchi zote mbili kwani Tanzania inalihitaji soko la Kenya kwa ajili ya Mazao ya wakulima wa Tanzania na nchi ya kenya inauhitaji na mazao mbalimbali hususani mahindi kutoka nchini Tanzania.
Ameeleza kuwa mkutano
huo pamoja na kujadili kuhusu vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru
utatoa fursa ya kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu Biashara ya
mazao na bidhaa zinazotokana na mazao.
“Tunakwenda katika mkutano huu tukiwa na agenda ya kuhakikisha kuwa tunaendelea kumkwamua mkulima wa Tanzania katika kutafuta masoko ya mazao kwenda Kenya vilevile ya Kenya kuja nchini” Amekaririwa Prof Mkenda.
No comments:
Post a Comment