Advertisements

Thursday, May 19, 2022

DKT. CHAULA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UN


Na WMJJWM- Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa (UN) Zlatan Millisic katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma Mei 18, 2022

Katika kikao hicho Dkt. Chaula na Mwakilishi Mkaazi wa UN Zlatan Millisic wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo uwezeshaji Wanawake kiuchumi, Usawa wa Kijinsia na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mikakati ya Utekelezaji wa Sera na Mipango mbalimbali ya kutoa huduma kwa wananchi.

No comments: