Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewaagiza Mawaziri wa Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango, kukutana na namna ya kuzungumzia miradi ya miradi ya kilimo ambayo ilianzishwa serikali ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa na tija yake ionekane kwa wananchi.
Ndugu Chongolo amesema hayo leo Juni 18, 2023 baada ya kukagua mradi wa Umoja wa Wakulima wa Zabibu wa ICHIMADA ulioko eneo la Chinagali, pamoja na Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa 'Jenga Kesho Iliyo Bora' (BBT) uliopo katika eneo hilo wilayani Chamwino mkoani. Dodoma.
Katibu Mkuu Chongolo amesema kuwa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuona miradi ya kilimo inaleta tija kwa haraka, hivyo ni muhimu miradi hiyo isiwe na majina mazuri tu, bali ilete matokeo na manufaa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment