Wednesday, January 24, 2024

BAADA YA MAANDAMANO WADADISI WA MAMBO WAISIFU SERIKALI KWA KUWAACHA WAANDAMANE NA SASA WAHOJI "WHAT NEXT???"

Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuandamana na kuwasilisha ujumbe wao Umoja wa Mataifa, wadadisi wa mambo wamehoji endapo kama kilichokusudiwa na chama hicho kimetimia ama kitatimia.

 

Wakiongea na VIJIMAMBO leo baada ya kile kilichoitwa Maajabu ya Mwaka kwa polisi kusindikiza maandamano hayo badala ya kuyashambulia kwa mabomu ya machozi na maji washawasha, wadadisi hao wamehoji endapo kama Umoja wa Mataifa ama Uingereza na Marekani ambako viongozi wa chama hicho walikwenda siku chacha zilizopita ndio wanayoendesha Tanzania.


Wengi wamehoji, 'What Next' (nini kifuatacho) baada ya kufanyika kwa maandamano hayo, wakisisitiza kwamba kama walitegemea kupata 'kiki' kwa njia hiyo basi wamenoa.

 

“Unajua CHADEMA wanadhani kulazimisha mambo kwa kutafuta sapoti ya vyombo na mataifa ya nje ni mbinu ya kujijenga kisiasa, wakati kumbe wamejichoresha kwa kuthibitisha kuwa yote haya wanafanya kwa kuwa sao ni vibaraka wanaotumiwa”, amesema Elias Mwikoloka wa Makongo juu.

 

Mwikolokwa ameungwa Mkono na wadadisi wengine kadhaa ambao hawajawahi kuona matatizo ya nchi yanatoweka kwa maandamano badala ya kukaa mezzani na kuamua kwa pamoja mstakabali wa chi yao.

 

“Ona wapinzani nchini Kenya walivyokubali matokeo na kusitisha maandamano bila masharti yoyote na hivi sasa serikali ya chi hiyo imeendelea kutatua matatizo yaliyopo moja baada ya lingine kwa utulivu”, amesema Bi. Aisha Swalehe, mfanyabiashara wa Kariakoo.

 

Bi Aisha amesema hata kama wapinzani wangeandamana hadi Kiama matatizo waliyoyataja yasingeondoka sana sana yangezidi, kwani maandamano ni stratejia ya kizamani ambayo kwa sasa haifanyi kazi tena, hasa kwa nchi za Kiafrika.

 

Wadadisi wengine wengi wameelezea kuchekeshwa na hatua ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kufika kwenye  maandamano na vijana aliodai  kuwa ni watoto wake, wakielezea kitendo hicho ni cha kitoto kwani (Mbowe) alijua fika safari hii polisi hawaji na mabomu na virungu ili kuwatawanya, bali watawasindikiza.

 

“Mbona wakati ule wa maandamano yaliyo yaliyosababishwa kufa kwa dada wa watu sio tu hakufika na watoto bali pia yeye mwenyewe alitoka mkuku baada ya kuona wanaume (askari). Asitufanye sie ni watoto bwana! “, amesema Mbwana ambae hakutaka jana lake la pili lijulikane kwa usalama wake.

 

Uchunguzi wa VIJIMAMBO umebaini kwamba safari hii serikali ya awamu ya sita imewapatia kweli CHADEMA ambao walijua watazuiwa hivyo vurugu ingetokea kwa wao kutaka kuandamana kibabe na kusababisha mabomu ya machozi na virungu kurushwa.

 

Imebainika pia kuruhusiwa kwa maandamano hayo kumwedhoofisha nia lao ya kutaka serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ionekane inaminya uhuru wa kuandamana hivyo kungekuwa na kelele nyingi kimataifa ambako misaada mingi hasa ya pesa hupatikana kwa wapinzani wanaoonewa.


Kuna wasiwasi pia kwamba kuitisha maandamano yao ni mojawapo ya mikakati ya CHADEMA kujipatia "kiki" ili kurejesha imani ya wanachama wao ambayo inasemkana imedidimia kwa chama hicho kupungukiwa mvuto na agenda za maana.


Vile vile hiyo inaonekana ni mkakati wa kuwavutia wanachama wake na kuungwa mkono katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na ule nuchaguzi Mkuu mwakani, baada ya CCM kutopoa na harakati za kuhamasisha umma bila kukoma na wao (CHADEMA) kuwa kimya

 




 

No comments: