Tuesday, January 23, 2024

CHADEMA YALIPIGIA SALUTI JESHI LA POLISI KWA KURUHUSU MAANDAMANO YAO LEO, CHAAHIDI KUTEKELEZA KILA WALILOKUBALIANA KATIKA KUDUMISHA AMANI NA USALAMA


Na Mwandishi wetu, Dar


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejivunjia rekodi yake yenyewe! Yaani kwa mara ya kwanza kabisa toka kianzishwe miongo mitatu na ushee  iliyopita kimelipongeza Jeshi la polisi kwa kuruhusu kufanyika kwa maandamano ya chama hicho  leo.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu (Bara) wa chama hicho Benson Kigaila kwa nyakati tofauti jana. 

 

Mbowe  ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa X wakati Kigaila alilipigia saluti kwa kulimwagia sifa jeshi hilo wakati anaongea na wanahabari mara tu baada ya kutoka makao makuu ya Kanda Maalumu ya Dar es salaam alikokuwa katika kikao toka saa tano asubuhi hadi saa tisa.

 

Mbowe jana ameandika: “Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa busara hii. Karibuni Watanzania wote, tuandamane kwa Amani…”

 

Mbowe ameanza kwa kueleza kwamba timu ya CHADEMA ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Bara Benson Kigaila imekuwa na kikao na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Dar Es Salaam ACP Jumanne Muliro na timu yake kuhusiana na Maandamano ya Amani yanayopangwa na kuratibiwa na CHADEMA siku ya Jumatano, 24 Januari 2024.

 

“Makubaliano yamefikiwa kuwa maandamano yaendelee kama yalivyopangwa”, amesema Mbowe kuhusu maandamano hayo ambayo hata hivyo, Polisi imeyakubali kufanyika kwa masharti kadhaa.

 

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo, Mrakibu Mwandamizi J.E. Josepha ameandika haya kwenye barua yace aliyoipeleka jana CHADEMA:

 

“Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu na rejea burua yako yenye Kumb:Na.C/ADM/MS/11/59 ya tarehe 16/01/2024.

 

“Kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu zinazohusu "taarifa za MAANDAMANO, hayatazuiwa na Jeshi la Polisi iwapo Maandamano hayohayataleta uvunjifu wa amani, au kusababisha kutendeka kwa vitendo vya kihalifu.

 

“Kwa barua hii viongozi wa CDM (CHADEMA) na wanachama mnalo jukuma la kuzuia lugha za uchochezi, kejeli zinazoweza kupelekea kutendeka kia vitendo vya uvunjaji wa sheria. 

 

“Mtalazimika kufuata utaratibu wa kisheria katika macneo yote kwa kadri mtakavyoelekezwa na wasimamizi wa sheria Polisi wakiwa ni kiongozi

katika eneo hilo mlilolitolea taarifa,

 

“Maandamano hayo yasisababishe uvunjivu wa amani/watu kuibiwa au kuporwa na yawe kwenye njia zilizokubaliva. 

 

“Taarifa yenu pia izingatie muda wa kilichoelezwa kwenye barua yenu ikiwa ni pamoja na kutoanzishwa mambo mengine ambayo hayamo kwenye taarifa iliyotolewa Polisi.

 

“Aidha, ukiukwaji wowote wa masharti hayo utalilazimisha Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria bila kusita ili kuzuia madhara ya kuvunjika kwa amani.

 

“Naamini msingi wa taarifa yenu utabaki kuwa ni kudumishwa kwa amani na utulivu uliopo nchini”, inamalizia barua hiyo.

 

Kwa Mujibu wa Bw. Kigaila maandamano hayo yatakuwa ya ruti (njia)  mbili kama ilivyopangwa. 

 

Amesema Ruti ya kwanza itaanzia Buguruni kupitia barbara ya uhuru hadi makutano ya barbara hiyo na ya Msimbazi, kisha watapinda kushoto na mwenda hadi makutano ya Msimbazi na barbara ya Morogoro Faya, kisha watapinda kushoto na kuyoosha hadi barbara ya Shekilango ambako watakutana na wenzao wa Ruti ya pili, na kwa pamoja wataingia barbara ya Shekilango hadi Sinza Makaburini barbara ya Igesa  hadi Sam Nujoma  na kurudi na barabara hiyo hiyo hadi ofisi za Umoja wa Mataifa  zilizo opposite na Mlimani City.

 

Bw. Kigaila amesema ruti ya pili itaanzia stendi ya mabasi ya Mbezi, itakayokuja na barbara ya Morogoro hadi makutano na  Shekilango  ambapo watakutana na wenzao wa ruti ya kwanza.

 

“Hayo yote tumekubaliana na pia jinsi ya kuendesha maandamano ya amani.

 

“Kwa naiba ya chama tunalipongeza Jeshi la Polisi. Kwa mara ya kwanza limeonesha weledi. Tumejadiliana na kuelewana. Tofauti na zamanı Jeshi la Polisi lilikuwa linachukulia kwamba sisi wanasiasa ama wasio polisi hatuna tunachokijua kuhusu usalama. 

 

“Lakini leo tumejadiliana na tumekubaliana na tuwapongeze. Na sisi kama chama tutawapa ushirikiano Wote kuhakikisha maandamano  yatakuwa ya salama. Tumekubaliana!

 

“Hivyo basi wanachama na wapenzi wa CHADEMA wakiona polisi kesho (leo) wasitishike kwani watakuwa wamekuja kuwalinda wakati wa maandamano hayo”, amesema Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.

 

No comments: