Advertisements

Wednesday, May 22, 2024

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOA WA KASKAZINI WILAYA YA KASKAZINI "B" UNGUJA


Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Othman Ali Maulid kulia akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Hamid Seif Said ili kuukimbiza katika Wilaya yake na kukagua miradi mbalimbali Zanzibar.
Muuguzi na Mkunga Wilaya ya Kaskazini B Firdaus Haji Omar akimpatia Chanjo Mtoto Nabil Khamis Idi katika Mradi wa Afya Chanjo na Matone Uliotembelewa na Mwenge wa Uhuru ili kuona Maendeleo na Mafanikio katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2024 Godfrey Elyakim Mzava akipima Ubora wa Jengo kwa kutumia Kifaa maalum (REBON HUMER)wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Ghorofa Bumbwini Kidazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Viongozi wa mbio za Mwenge wakiingia katika Shamba la Mradi wa Vijana waliojiajiri Vanila Growing Operetive ili kuangalia maendeleo yake na Changamoto Shehia ya Donge Mbiji Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Ali Issa. Maelezo
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Godfrey Eliyakim Mzava amewataka Vijana kushiriki katika kilimo cha vanilla na spice ili waweze kujipatia kipato cha kuendesha Maisha yao ya kila siku.

Amesema hayo wakati wa ukaguzi wa mradi wa shamba la vanilla na viuongo vya utalii (spices) huko Donge mbiji wilaya kaskazini B.

Amesema zao hilo linathamani na tija kubwa hivyo ni vyema kutumia fursa hiyo ili waweze kujikomboa na kuepukana na tatizo la umasikini.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Dongo Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema shamba hilo linapokea watalii wengi kwa kufanya utafiti na kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia kilimo hicho.

Dkt. Khalid ambe pia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi amesema shamba hilo ni kielelezo cha kuimarisha bidhaa za utalii hapa nchini na kuwapatia kipato wananchi wa Donge na maeneao ya Jirani.

Aidha amemshakuru kiongozi wa mbio za mwenge kwa kufika jimboni humo na kuweza kukagua mradi mbalimbali ya maendeleo jambo ambalo limezidisha ari na hamasa kwa wananchi kushiriki katika harakati za maendeleo.

Mapema akisoma risala ndg. Khamis Dola Khamis amesema shamba hilo lina ukubwa wa ekari 12 na linauwezo wa kuzalisha zaidi ya sh. milioni 19 kwa kilo 65 kavu.

Amefahamisha kuwa soko la kuuzia bidhaa hizo lipo kwani tayari Kampuni kutoka Ujerumani imekubali kununua bidhaa zao wanazozizalisha.

Amebainisha kuwa ushirika huo, unapokea vijana kwa kuwapa taluma ya kilimo cha vanilla, spice, na bidhaa mbalimbali ikiwemo Tangawizi, Mchaichai, Karafuu na Bizari.

Mradi huo,umeazishwa Mwaka 2017 na unathamani ya zaidi ya sh. milioni 100 na upo katika maeneo mbalimbali kama vile Mangapwani, Chechele na Karange.

No comments: