Advertisements

Wednesday, May 22, 2024

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI NA UNICEF MAKUBALIANO YA MANUNUZI


Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazurui akizungumza katika Hafla ya utiajibsaoni mkataba wa manunuzi Kati ya Wizara hiyo na UNICEF kupitia mradi wa uwekezaji wa huduma ya mama na mtoto (TMCHIP) wenye thamani ya dola za kimarekani 12,500, 000 huko Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.

Na Fauzia Mussa - Maelezo
Wizara ya afya Zanzibar imetiliana saini na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto ulimwenguni (UNICEF) mkataba wa manunuzi wenye thamani ya USD-12,500,000 Sawa na zaidi ya shilingi bilioni 30.

Mkataba huo uliotiwa saini na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Habiba Hassan Omar na Mwakilishi mkaazi wa UNISEF Nchini Tanzania Elke Wisch ni miongoni mwa utekelezaji WA mradi wa uwekezaji wa huduma ya mama na mtoto( TMCHIP) unaofadhiliwa na benki ya dunia wenye Lengo la kuimarisha Afya ya uzazi Kwa mama na mtoto.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini mkataba huo huko golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar Waziri wa Wizara hiyo Mhe Nassor Ahmed Mazurui amesema Wizara ya Afya imeingia makubaliano na UNICEF kununua vifaa tiba ili kupata vifaa vyenye ubora, uimara na kwa urahisi.

Amesema endapo vituo vya Afya ya Msingi vitaimarishwa kutasaidia kuimarisha Afya ya mama na mtoto na kupunguzo Vifo vitokananvyo na uzazi.

Mbali na hayo mkataba huo utahusisha manunuzi ya teknolojia za mawasiliano ili kuviunganisha vituo 52 vya Afya ya Msingi pamoja na kununua vifaa tiba vya hospital hizo na benki ya Damu.

Aidha ameeleza kuwa kupitia mradi huo wafanyakazi wa Afya ngazi ya jamii CHW watapatiwa mafunzo maalum kuhusiana nalishe ili kuwaelimisha akina mama juu ya kujenga Afya zao kwani Vifo vingi husababishwa na Ukosefu wa lishe unaopelekea upungufu wa Damu.

Waziri mazrui alisema kuwa Serikali itahaliksha inahusisha na kuwafikia walengwa wote Hadi kuona malengo ya mradi huo yanafikiwa.

"UNISEF watatunulia vifaa mbalimbali kupitia Fedha hii tuliowakabidhi ikiwemo vifaa tiba,madawa magari ya kubebea wagonjwa vitakavyotumika katika vituo vya ya Msingi Lengo ikiwa ni kuimarisha Afya ya mama na mtoto." Alisema mazrui.

Kwaupaande wake Mwakilishi mkaazi wa UNISEF Nchini Tanzania Elke Wisch amesema mradi huo utahakikisha mama wote na Zanzibar wanakua salama kutokana na Afya ya uzazi mradi wa uwekezaji wa huduma ya mama na mtoto( TMCHIP) ulianza 2023 na kutarajiwa kukamilika 2027.

No comments: