Thursday, October 24, 2024

UN IMECHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KATIKA ENEO LA USTAWI KWA JAMII KATIKA NYANJA MBALIMBALI


Na Hawa Abdallah
MRATIBU wa Umoja wa Mataifa Ofisi Ndogo Zanzibar Derothy Temu-Usiri amesema UN imechangia kwa Kiasi kikubwa Katika eneo la ustawi kwa Jami katika nyanja mbalimbali kupitia mashirika ya umoja huo.

Mratibu huyo aliyasema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa kila ifikapo Oktoba 25, mkutano uliofanyika katika Ofisi zake huko Kinazini.

Kauli mbiu katika maadhimisho ya Mwaka huu 2024, ni Ustawi kwa Vizazi vijavyo: Kuendesha Ukuaji endelevu nchini Tanzania.

Alisema kauli mbiu hiyo inakwenda sambamba na shughuli ambazo shirika hilo linafanya kwa kupitia mashirika yao mengine na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Alisema shirika hilo linafanya kazi na mataifa 196 pamoja na kushiriki katika ulinzi wa Amaan pamoja na kishughulikia mizozo katika nchi ambazo wanafanya kazi.

Alisema katika kuhadhimisha siku hiyo muhimu hasa kwa mwaka huu 2024, UN imetafakari maadili ambayo yameongoza shirika hilo kwa miaka 79.

Nae Afisa wa Programme za jinsia wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA Ali Haji alisema ndoto ya shirika hilo ni kuhakikisha upatikanaji wa haki ya Afya ya Uzazi, uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana na usawa wa Kijinsia.

Alisema kuelekea 2030 UNFPA Tanzania na Zanzibar Ibadan ya kazi kutimiza malengo manne muhimu.

Aliyataja mambo hayo ni hakuna mahitaji yasiyotimizwa ya taarifa na huduma za Uzazi wa mpango.

Jambo jingine pasiwepo na Vifo vya uzazi vinavyoweza kuzuilika, pasiwepo na udhalilidhaji na ukatili wa Kijinsia na pia mila potofu pamoja na pasiwepo na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Katika Mkutako huo wawakilishi kutoka UNICEF, FAO na UNOPS nao waliwasilisha mafanikio waliyoyapata kupitia mashirika yao katika kuelekea siku ya Umoja wa Mataifa.

No comments: