Friday, October 25, 2024

WANANCHI JIJINI MBEYA WAIPONGEZA SERIKALI KUSOGEZA ELIMU YA FEDHA KARIBU


Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (Kushoto), akimweleza Mkazi wa Jiji la Mbeya, Bw. Albert Mwaipogole, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Mchumi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Felista Malibate (Kulia), akitoa elimu ya fedha kwa Mkazi wa jiji la Mbeya, Bi. Mary Mpombo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Mhasibu Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bi. Kurthum Juma, akitoa elimu kuhusu masuala ya madeni ya Serikali kwa baadhi ya wananchi wa Jiji la Mbeya, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Mchumi kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bi. Anna Ndagile, akiwaeleza baadhi ya wananchi wa jiji la Mbeya, kuhusu Dondoo Muhimu za Sera za Kodi, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Cosmas Nshenye (Kushoto), akiwaelezea Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwakibete, kuhusu masuala ya Bajeti ya Serikali, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Mtaalamu kutoka Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. George Killo (kushoto), akimmonesha Mkazi wa Jiji la Mbeya, Bw. Selemani Ndelage, kipeperushi chenye maelezo kuhusu namna wanavyosimamia mali za Serikali, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mbeya)

Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Mbeya
Wakazi wa Jiji la Mbeya wameipongeza Serikali kwa kuwasogezea elimu ya fedha na huduma mbalimbali za fedha karibu nao.

Wametoa pongezi hizo katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya.

Wamesema elimu wanayoendelea kuipata katika maadhimisho hayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wao binafsi na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Bi. Rehema Kassiba wa Kumekucha Saccos ni miongoni mwa wananchi hao, alisema maadhimisho hayo yamewarahisishia upatikanaji wa elimu na huduma za fedha kwa kuwa Serikali imezisogeza huduma muhimu za masuala ya fedha katika maadhimisho hayo.

Aliipongeza Serikali kwa kuandaa maadhimisho hayo na kuahidi atakuwa balozi mzuri kwa kuifikisha elimu aliyoipata kwa wananchi wengine ambao hawajapata nafasi ya kufika viwanjani bua Nzowe yanapofanyika maadhimisho hayo.

“Elimu hii ni nzuri na muhimu kwetu lakini tunaiomba Serikali iandae utaratibu wa kufikisha elimu hii katika maeneo ya vijijini kwa kuwa muda wa maadhimisho haya ni mchache sio rahisi kwa wananchi wote kuhudhuria hususan wale wanaotoka vijijini”, alisema Bi. Kassiba.

Naye Bw. John Mwakipasile, Mjasiriamali wa soko la Mwanjelwa alisema maadhimisho hayo yamewaongezea uelewa wa fursa mbalimbali zinazopatikana katika Sekta ya Fedha.

Alisema katika maadhimisho hayo wamepta ujuzi wa matumizi sahihi ya huduma za fedha katika kukuza biashara zao, utamaduni wa kujiwekea akiba, kukopa na kulipa madeni.

Kwa upande wao, Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Mbeya, nao wameishikuru Serikali kwa kupeleka Maadhimisho hayo jijini hapo kwa kuwa yamewawezesha kuwapata wananchi wengi ndani ya muda mfupi.

Mratibu wa Mikopo wa Jiji la Mbeya, Bi. Aksa Njidile ni miongoni mwa Maafisa hao, ambaye aliwakaribisha wananchi kwa kutembela maadhimisho hayo ili wapate elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa.

Alisema wakitembelea katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine, watapata elimu ya mikopo mbalimbalimbali inayotolewa na Serikali hususan ile ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.

Naye Afisa Vijana wa Jiji la Mbeya, Bi. Ritha Mushi amewahamasisha vijana wa Jiji hilo kutembelea maadhimisho hayo ili watapate elimu ya fursa mbalimbali za kujiinua kiuchumi zinazotolewa na Serikali.


Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanatarajia kuongeza idadi ya watu wenye elimu ya fedha na maarifa juu ya upatikanaji na utumiaji wa bidhaa na huduma rasmi za kifedha pamoja na kuongeza mchango wa Sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa uchumi.

No comments: