ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 25, 2010

Angola yataka idhini ya kuchimba mafuta DRC


 
 Bunge nchini Angola limeidhinisha mashauriano yafanyike kati ya serikali hiyo na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kabla ya kuomba Umoja wa Mataifa kupanua mipaka yake baharini.
Angola inanuia kupanua shughuli zake za kuchimba mafuta kwa zaidi ya maili 300 baharini lakini lazima kwanza ipewe idhini na Congo. Awali Congo ilishutumu Angola kwa kuiba mafuta katika ufuo wake.
Afisa kutoka serikali ya Congo amesema kuwa nchi hizo mbili zitajadiliana kuhusu muafaka wa pamoja mwezi ujao.

No comments: