ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 25, 2010

Polisi Kenya walaumiwa kuwatesa wakimbizi


  
Mashirika ya kutetea maslahi ya wakimbizi, yamewalaumu polisi nchini Kenya kwa ukiukaji wa haki za wakimbizi.
Mashirika hayo, Refugee Consortium Of kenya, Humanitarian Policy Group (HPG), na International Rescue Committee (IRC), yanasema polisi wanawatesa maelfu ya wakimbizi wanaotafuta hifadhi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
''Polisi, wanawalazimisha kulipa pesa, wanawakamata, na kuchana nyaraka za wakimbizi'', Alisema afisa wa shirika la Refugee Consortium Of Kenya Simon Konzolo katika mahojiano na BBC.
Mashirika yanayotetea haki za wakimbizi yametoa ripoti ya pamoja itakayotolewa rasmi kwa umma hii leo kuhusu unyanyasaji huo na namna ya kukabiliana nao.
Zaidi ya wakimbizi elfu 46 wamesajiliwa mjini Nairobi .

No comments: