
Baada ya siku mbili za mashauriano mjini Washington, juhudi za Israel kukomboa uhusiano wake na Marekani zimegonga mwamba.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekutana na rais Barack Obama na mjumbe wake wa mashariki ya kati George Mitchell lakini bila mafaniko yoyote.
Marekani imesisitiza kwa Israel ifanye juhudi za kuaminika katika kurejesha imani kwa mashauriano ya amani kati yao na Palestina. Hata hivyo hakuna ishara zozote kwamba Netanyahu amekubaliana na hayo.
Marekani imeghadhabishwa na hatua ya Israel kujenga makaazi mapya ya wayahudi katika eneo la Jerusalem Mashariki ambayo wamesema inahujumu juhudi zake kutafuta amani katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment