ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 24, 2010


Mgao wa umeme kwishne!

tanescotop  
Hatimaye mgawo wa umeme ambao ulisababishwa na kuharibika kwa mitambo kwenye mabwawa manne, sasa umekwisha baada ya mafundi kufanikiwa kuirekebisha.

Hayo yaliwekwa wazi jana na Waziri wa Nishati na Madini..."Nadhani Tanesco wameshatolea maelezo hilo... mgao haupo kwa kuwa umeme wa mitambo ya Kihansi na ile nyongeza ya IPTL uko kwenye gridi ya taifa hivi sasa," alisema.

Ngeleja ametoa kauli hiyo wiki moja baada ya Tanesco wiki iliyopita kutangaza kuanza kwa mgao kwenye mikoa yote kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa umeme kwenye baadhi ya vituo vya uzalishaji.

Mgawo wa umeme umekuwa ukirejea kila mara licha ya Tanesco kutangaza kukomesha tatizo hilo, kutokana na uzalishaji kulingana na mahitaji na hivyo kutokuwa na akiba ya kuweza kuziba upungufu unaosababishwa na kuharibika kwa baadhi ya mitambo.

Tanesco jana mapema asubuhi walithibitisha kuisha kwa mgao huo na kuwahakikishia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwamba wataendelea kupata huduma hiyo bila bughudha

No comments: