Serikali ya Saudi Arabia inasema inawazuilia watu wapatao 100 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wenye uhusiano na kundui la Al-Qaeda.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema raia 47 wa Saudi Arabia, na raia wengine 51 wa kigeni wakiwa katika makundi matatu tofauti walikuwa wanapanga njama za kushambulia vituo muhimu vya mafuta na vikosi vya usalama.
Msemaji huyo amesema makundi hayo yana funganisho na tawi la al-Qaeda lenye ngome yake katika nchi jirani ya Yemen.
Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa ikishuku kuwa kundi la Al Qaeda hivi sasa linatumilia machafuko katika Yemen ili kufanya mashambulizi dhidi dola hiyo ya kifalme na mataifa mengine ya eneo hilo.
No comments:
Post a Comment