ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 24, 2010

Akon marufuku Srilanka


Sean Kingston, John Mayer, Pete Wentz, Corrine Bailey Rae, Gavin DeGraw, Alison Iraheta, Kesha and Akon out and about in New York City.  
Serikali ya Sri Lanka imempiga marufuku mwanamuziki wa kimataifa kutoka Marekani, Akon, kuingia nchini humo kufuatia maandamano yanayopinga kanda yake ya video inayoonekana kukejeli dini ya Budha.
Mwanamziki huyo mzaliwa wa Senegal alitarajiwa kuandaa tamasha lake kubwa mjini Colombo mwezi Aprili.
Video hio ya wimbo , Sexy Bitch, inaonyesha watu waliokusanyika karibu na bwawa la kuogelea kwa karamu maalum nyuma yake ikionekana sanamu ya Buddha .
Taarifa ya serikali ya Sri Lankan imesema kuchanganya sanamu hiyo ya Buddha pamoja na wanawake waliovalia mavazi yasio na sitara kumewasikitisha wafuasi wa Buddha kila mahali kwa hiyo maombi ya Akon ya kupewa visa hayatakubaliwa.
Zaiara yake ambayo ilitumainiwa ingewavutia mashabiki kutoka nchi nyingine za Asia imekwishazusha mgogoro mkali. Kundi la watawa wa kihafidhina limesema video za Akon hazifai kwa nchi yenye wafuasi wengi wa Budha kwa sababu inachochea hisia za ngono.
Mnamo siku ya Jumaatatu takriban watu 200 waliyashambulia kwa mawe na chupa makao ya kampuni moja iliyohusika na kuitangaza ziara ya Akon.
Akon amesema yeye ni mtu wa kidini ambaye kamwe hatathubutu kukashifu imani ya kidini ya mtu yeyote.

No comments: