ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 27, 2010

Ajali ya Kibamba yaua familia moja

Image
Mtoto Mwanaidi Ibrahim (4) (kulia), ambaye wazazi wake wote wawili walifariki dunia katika ajali ya gari, Kibamba juzi, akiwa amebebwa na Mama yake mdogo, Sharifa Ally wakati wa maombolezo ya msiba wa wazazi wake hao, Kibamba, Dar es Salaam jana. Kushoto ni ndugu yake Salha Jaffar (3). Mtoto huyo kwa sasa amebaki yatima. (Picha na Fadhili Akida).
AJALI ya lori na basi dogo iliyotokea juzi Kibamba, Dar es Salaam iliua watu wawili wa familia moja akiwamo mjamzito na kusababisha mtoto mwingine kubaki yatima, imebainika.

Waliokufa ni mjamzito na mumewe ambaye alikuwa akimsindikiza mkewe siku hiyo kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhudhuria kliniki.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu wa kiume, Issa Ngoro, kaka yake kwa jina la Ibrahim Hussein Ngoro na mkewe Zainab Ali aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane ndio waliokumbwa na janga hilo.

Issa alisema kaka yake alikuwa mfanyakazi katika bandari ya Dar es Salaam na alikuwa na kawaida ya kudamka kuwahi kazini akichelea msongamano wa magari barabarani.

“Siku ya tukio, aliondoka alfajiri sana akifuatana na mkewe ili ampeleke kliniki Muhimbili kwanza ili kuwahi foleni ya wajawazito Muhimbili na barabarani na kisha naye awahi kazini kwake,” alisema Issa.

Alisema familia hiyo imeacha mtoto mmoja wa kike, Mwanaidi Ibrahim (4) na mimba aliyokuwa nayo ilikuwa ya uzao wa pili.

Aliongeza kuwa taarifa za ajali hiyo alizipata akiwa msikitini asubuhi, ambapo Imamu aliwatangazia kuwa kuna ajali eneo la darajani na kumlazimu kwenda kushuhudia ingawa hakuwa na uhakika kama alikuwamo ndugu yake.

“Nilipofika pale kwa kweli nilichanganyikiwa kwa jinsi maiti walivyokuwa wamekatikakatika na baada ya kuona mjamzito akitolewa, ndipo nikamwaza shemeji yangu, na baadaye kidogo nikaona mguu wa kaka ukitolewa na niliutambua kwa kuwa ulikuwa na kovu kwa nyuma,” alisema Issa.

Issa aliongeza kuwa baada ya hapo, alimpigia kaka yake simu ambayo ilikuwa haipatikani, na baadaye ikambidi arudi nyumbani huku akiogopa kumwambia mama yao na walipopiga simu ya shemeji yake ikapokewa na polisi na kuarifiwa kuwa anayepigiwa amekufa na yuko mochari

No comments: