
Rais Barack Obama(shoto) na Rais Dmitry Medvedev
Rais Barack Obama na Rais Dmitry Medvedev wamekubaliana juu ya mkataba mpya wa kupunguza silaha za nuclear baada ya miezi kadhaa ya majadiliano.
Makubaliano haya yanaashiria hatua muhimu ya sera za nje kwa rais Obama. Haya ni makubaliano ya kwanza ya kina kuhusu silaha za nuclear, tangu makubaliano yajulikanayo kama START yaliyofikiwa mwaka 1991.
Upunguzaji wa silaha katika makubaliano haya si mkubwa, lakini ni muhimu. Pande zote mbili zitasalia kuwa na silaha nyingi.
Lakini makubaliano haya mapya ambayo yatatiwa saini mjini Prague yanaashiria hatua ya kwanza katika mipango ya rais Obama ya kudhibiti silaha.
No comments:
Post a Comment