
WIMBO kwenye kambi ya Simba mjini hapa ni “ushindi kama nyumbani”.
Simba ipo mjini hapa kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DC Motemba Pembe, mechi itakayochezwa kesho.
Kauli hiyo ya Simba inatokana na kupewa hamasa na mashabiki wa timu za As Vita na Emana za mjini hapa kwamba kesho wataiunga mkono asilimia 100.
Simba ipo mjini hapa kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DC Motemba Pembe, mechi itakayochezwa kesho.
Kauli hiyo ya Simba inatokana na kupewa hamasa na mashabiki wa timu za As Vita na Emana za mjini hapa kwamba kesho wataiunga mkono asilimia 100.
Katika kudhihirisha hilo, mashabiki wa timu hizo jana walifurika katika mazoezi ya Simba kwenye uwanja wa Shark huku wakitamba watakuwa upande wa Simba.
“Hili limetufariji sana, tunaona kama tupo nyumbani,” alisema nahodha wa Simba, Nicodemus Nyagawa. Alisema mara nyingi wachezaji wanapokuwa ugenini huingia woga kutokana na mashabiki kutokuwa upande wao ila sasa wamepata nguvu.
Upinzani wa Motema Pembe na Vita ni kama wa Simba na Yanga kwa Tanzania. Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema ari ya wachezaji iko juu na wamewahamasisha vya kutosha.
“Tumefarijika pia kuona wapinzani wetu wanachukiwa…Watanzania wasubiri kuipokea Simba Jumatatu (keshokutwa) ikirejea ikiwa imeingia hatua ya makundi,”alisema.
Mechi hiyo itachezwa kesho kwenye uwanja wa Stade De Marthy kuanzia saa tisa alasiri kwa saa za huku ambapo ni sawa na saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watazamaji 90,000 ambao ni pamoja na waliokaa na kusimama.
Akiizungumzia mechi hiyo, Kocha mkuu wa Simba Moses Basena alisema mipango ya kushinda imeshakamilika, jukumu limebaki kwa wachezaji.
Simba inahitaji ushindi au sare yoyote kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo. “Kila kitu nimeshamaliza, najivunia kuwepo kwa Jerry Santo katika mechi hii kwani ataimarisha kikosi,” alisema.
CHANZO:HABARI LEO
No comments:
Post a Comment