ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 30, 2011

Kanisa la Synagogue Church of All Nations watoa Mil.25/- kusaidia waathirika wa Ajali ya Meli MV Spice Islander

Mwakilishi wa Emmanuel Televisheni  na Kanisa la The Synagogue Church  Of All Nations Bi. Martha Harvey akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jumla ya shilingi milioni ishirini na tano 25,000,000/- kwaajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander  iliyozama katika mkondo wa Nungwi huko Unguja na kusababisha vifo vya watu wengi hivi karibuni. Mchango huo uliokabidhiwa leo ikulu jijini Dar es Salaam umetolewa na Kiongozi wa Kanisa hilo Nabii Themitope Balogun Joshua ambaye anaishi katika MAKao makuu ya Kanisa hilo jijini Lagos Nigeria.
 Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

No comments: