Advertisements

Saturday, September 10, 2011

MELI YA SPICE ISLANDERS YAZAMA PWANI YA NUNGWI IKIELEKEA PEMBA

MELI ya Spice Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea bandari ya Malindi Unguja.
Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo zinaendelea hivi sasa.
Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku.
Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa.
Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki, lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.
Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi kama boti ziendazo kasi vimekwenda eneo la tukio kutoa msaada. Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helikopta yake kwenye eneo la tukio.
Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio. Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

Rais wa Zanzibar na Barazra la mapinduzi Zanzibar,Dr Ali Mohamed Shein(katikati)akiwa na makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa kwenye huzuni mara walipofika kwenye eneo la tukio la ajali ya meli ya Spice Islander iliyozama katika bahari ya Nungwi,Mkoa wa Kasikazini Unguja
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbalimbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ufukwe wa bahari ya Nungwi,usiku wa kuamkia leo
Balozi Seif Ali Idd akitoa maelakezo juu ya utaratibu utakaofutwa kwa watu watakao kuja kuangalia maiti za wapendwa wao ndani ya hema hilo tayari kwa kuwatambua ndugu zao,katika  maandalizi hayo idara ya maafa wakishirikiana na Ofisi ya Mufti a Zanzibar watazihudumia maiti zote kwa kuzikosha,kuzivika sanda na kuzizika(picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

No comments: