ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 13, 2011

Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru Zimetingisha Mji wa Berlin

 Balozi Ngemara akiwa na viongozi wa UTU
 Balozi Ngemera (katikati) akiwa na viongozi wa Umoja wa watanzania Ujerumani UTU
 kikamada ketu Ras Makunja wa FFU alikuapo
 Ras Makunja na mzimu wake wa Ngoma Africa band
 washambuliajji wa magitaa wa FFU wakipakua vitu
 watanzania ujerumani hakubaki mtu nyumbani hadi watoto wachanga
watanzania ujerumani wakijipendelea
Ubalozi na Watanzania wafanya kweli Ujerumani !
 
Ngoma Africa Band aka FFU ! wamedatisha waheshimiwa na wadau  wote !
 
 
Berlin,
 
Siku ya ujumaa ya 9.12.2011 na jumamosi 10.12.2011 Watanzania waishio Ujerumani na nchi jirani
wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani,walifanikiwa kulitingisha jiji la Berlin "!
katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, sherehe hizo zilizoongozwa na Balozi
Bw.Ngemela na maofisa wa ubalozi akiwemo Bw.Ali Siwa zilianzia katika ukumbi wa Martim
ambako kulikua na mkusanyiko wa mabalozi wa nchi mbali mbali,vingozo wa ngazi za juu wa
serikali ya Ujerumani,watanzania, mashirika NGO's,na marafiki wahisani wa Tanzania walikuapo
kusherekea na kuipongeza Tanzania kwa kufikia miaka 50 ya uhuru kwa amani, Tanzania pia
ilipongezwa na kutajwa kuwa nchi ya Amani barani afrika ambayo wananchi wake wameshikama
kwa amani na upendo.
 
Ngoma Africa Band aka FFU chini ya uongozi wake Ras makunja aka Kamanda wa FFU,
muziki wa bendi hiyo ulifanaikiwa kuwachanganya uwanjani madipromasia na wadau walioudhuria katika sherehe hizo ijumaa na jumamosi bendi hiyo maarufu inatamba na
CD mpya  Shangwe 50 Uhuru anniversary.

Pia sherehe hizo ziliambata na ufunguzi wa chama cha Watanzania ujerumani (UTU) ambacho
kilifunguliwa rasmi siku ya jumamosi 10.12.2011 na Balozi  Mhe.Ngemera ambaye pia ndie
aliyetilia mkazo kwa kuanzishwa kwa umoja huo ambao ndio mwavuli wa watanzania wote
waishio Ujerumani,Umoja huo umesajaliwa na serikali ya Ujerumani kama NGO's na mwenyekitiki wake Bw.Mfundo Peter Mfundo.
 

No comments: