ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 9, 2011

TANZANIA INVESTMENT FORUM 2011



Wizara ya Nishati na Madini ikishirikiana na ubalozi wa Tanzania Uk wameandaa kongamano la uwekezaji nchini. Hii ni katika kutekeleza sera za economic diplomacy pamoja na kuvutia mitaji ya kigeni. Mada nyingi zilizungumziwa kuhusu nafasi na sheria za uwekezaji Tanzania. Waziri Ngeleja kama mgeni rasmi na mwakilishi wa taifa aliwawekea wazi wawekezaji jinsi ya sheria mpya zilizotungwa na kuwahakikishia kuwa Tanzania na Watanzania wako tayari kupokea wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza ilimradi waje na njia ambazo hazitinyinya Watanzania na taifa lao.

Eneo lililovutia sana washiriki lilikuwa eneo la nishati na madini pamija na viwanda. Waekezaji ambao tayari wako nymbanu Tanzania wamwisifia sana kwamb kwasasa Tanzania inawezekana kuwa ndio nchi pekeweafrika yenye mazingira sawia  kwa wawekezaji toka nje. Wanataaluma nao kama bi Barbara Njau alifafanua kwa ushahidi wa vielelezo kuwa uchumi Watanzania siku zijazo utakuwa haraka sana na yakuwa Watanzania na Tanzania wako kwenye nafasi nzuri kabisa kimaendeleo kama watatumia rasilimali walizonazo kwa umakini na uangalifu.
 Balozi Peter Kallaghe akitafakari yasemwayo kwa umakini
 Dr Abdelhelm Meru Mkurugenzi mkuu wa EPZA akitoa mada iliyosisimua kuliko zote
 Mh ngeleja akibadilishana mawzo na Naibu Balozi chabaka na Moja ya wanakongamano
 Mh Ngeleja akitoa maelezo juu ya sheria mpya za uwekezaji kwenye eneo la nishati
Waziri Ngeleja akiwa na Wajumbe wa JumuiyaTanzanian Uk
  . 
Asanteni,

Urban Pulse Creative

No comments: