ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 9, 2011

UNIC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA JUU YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA KULINDA HAKI ZA BINADAMU

Afisa Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika  katika Ofisi za UN Information Centre.
Human Rights Learning Program for Youth on Use of Social Media to Advocate For Human Rights imeandaliwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kwa Kushirikiana na Taasisi ya Under the Same Sun
Afisa  Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusiana na Azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwaka  1948 lenye vipengele 30 ambavyo vimeainisha Haki Msingi za Binadamu na Uhuru.
Mtaalamu wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka  Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG  Bw. Ayoub Rioba na Afisa  Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo.
Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG  Bw. Ayoub Rioba akielezea nafasi ya vijana kama wahusika wakuu katika matumizi ya Mitandao hiyo ambapo amewataka vijana kuwa watetezi wa haki za Binadamu kwa kutoa taarifa pale wanapoona haki hizo zinakiukwa.
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Vicky Ntetema kutoka Taasisi inayotetea haki za jamii ya watu wenye Ulemavu wa Ngozi ya Under the Same Sun akieleza jinsi watu wengine wanavyoweza kutumia mitandao hiyo kukiuka haki za msingi za Binadamu kwa namna mbalimbali na kuwataka vijana kuwa makini na kuepuka kupeana ahadi za kukutana na watu wasiowajua waliowasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Blogs.
Pamoja na mambo mengine Ntetema amewaasa vijana hao pamoja na jamii nzima kwa ujumla kutowaita watu kutokana na ulemavu walionao bali watumie majina yao halisi akitolea mfano kuwaita watu wenye ulemavu wa ngozi "Zeruzeru" (Albino).

Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Chang'ombe, Ruvu Sekondari, IST, Kibasila, Loyola na TEYODEN wakifuatilia mafunzo hayo.

Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Janeth Absalom kutoka Loyola High School akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Habari wa Temeke Youth Development Network (TEYODEN) Humphrey Shao akifafanua jambo kuhusiana na matumiz ya mitandao kama njia ya mawasiliano.

Wanafunzi wakifuatilia mafunzo hayo.


Pichani Juu na Chini ni Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
Kwa picha zaidi na maelezo Bofya Read more

 Mkurugenzi wa Mafunzo na  Elimu kwa Umma wa Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Rosemary Jairo akiwataka wanafunzi kutoa mapendekezo ni namna gani wataweza kusaidia kufikisha ujumbe kiurahisi kwa jamii kuhusiana na Haki za Binadamu ambapo pia amewataka wanafunzi wote waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mabalozi katika kutetea haki za Binadamu kama zilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kwa kufikisha ujumbe kwa wenzao na katika jamii inayowazunguka.
Wanafunzi wakiwa wameshika Poster yenye Ujumbe maalum unaonyesha kwamba Binadamu wote ni sawa bila kujali aina ya Ulemavu mtu alionao.
Afisa Habari wa United Nationa Information Centre Usia Nkhoma akigawa nakala za Filamu ya "White and Black: Crimes of Color". kwa wanafunzi wawakilishi wa shule zilizohudhuria mafunzo hayo.
(Picha kwa hisani ya MO Blog)

No comments: