Ndugu zangu Watanzania wenzangu hususani wanaDMV, kesho Jumapili Feb 12, 2012 tutakuwa na harambee ya kujaribu kuchangisha pesa za kusaidia mazishi ya ndugu yetu, mtanzania mwenzetu, mpendwa wetu, mama wa watoto wawili miaka 4 na miaka 2 na mke wa Lavorn Cryor.
Gharama za Funeral Home na mazishi ya mpendwa wetu zinafikia $ 11,000/ na michango iliyochangwa mpaka sasa ni $5,000/ bodo tunasafari ndefu na kukukumbushana kuwa msiba huu ni wetu sote tunaomba tujitokeze kwa wingi kesho tuweze kufanikisha na hatimae kuwezesha maziko ya Mtanzania mwenzetu na mpendwa wetu Christavina Cryor.
Kama unachochote unachoona kinaweza kunadiwa tafadhali njoo nacho, Harambee ni saa 8.30 mchana (2.30pm).
Anuani ni:
3621 Campus Drive,
College Park, MD 20740.
Kwa wale wa mbali au wasioweza kuhudhuria tafadhali tusaidie mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 25507198 Jina la A/c ni Lavorn Cryor. Tafadhali eneza habari hii kwa ndugu na marafiki wote. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu katika wakati huu mgumu.
Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile(240.938.3177); Teddy (301.254 1696); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca (240 898 7161).
****************************R. I.P Christavina*************** *************
No comments:
Post a Comment