![]() |
| MBUNGE wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF) |
Hebel Chidawali, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF) ameliamba siri bungeni kuhusu alivyodhalilishwa gerezani kwa kuvuliwa nguo zote.
Sakaya na wenzake 11 walikamatwa wilayani Urambo, Mkoani Tabora Juni 2011 baada ya kutuhumiwa kufanya mkutano wa hadhara bila kibali na baadaye kufikishwa mahakamani, lakini walikosa dhamana na kusota rumande kwa wiki mbili.

Sakaya aliliambia Bunge jana alidhalilishwa na askari wa magereza akiwa gerezani kwa kuamriwa kuvua nguo zote.
Alisisitiza kwamba, atakuwa mtu wa kwanza kutoa ushahidi popote kuhusu vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na askari magereza dhidi ya wafungwa na hasa wa kike.
Mbunge huyo alitoa madai hayo baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Khamis Kagasheki kueleza kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuwapo wa wanawake wanaoteswa na kudhalilishwa gerezani.
“Mheshimiwa spika, mimi ni shahidi namba moja katika jambo hilo, maana nimekuwa miongoni mwa wahanga hao na kwamba jambo hilo lipo. Wanawake wanavuliwa nguo hadi ya mwisho na kubaki uchi wa mnyama,’’ alidai Sakaya na kuendelea:

“Mheshimiwa spika, wanatafuta ushahidi wa aina gani, mimi ni shahidi namba moja wala wasipate tabu nitawapa ushahidi wote kule wanawake wanavuliwa nguo na kupata mateso makali.’’
Sakaya alitoa dukuduku lake alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kutokana na swali la msingi lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mhonga Ruhwanya.
Swali la msingi
Ruhwanya alisema askari magereza wamekuwa wakiwanyanyasa na kuwadhalilisha wafungwa wanawake, hivyo alitaka kujua Serikali inawachukulia hatua gani kwa askari magereza wanaowadhalilisha wafungwa wanawake kwa kuwavua nguo na kuwaacha wakiwa uchi wa mnyama kabla ya kuwarusha kichura chura.Ruhwanya alisisitiza pia kuwa upo ushahidi wa kutosha kutoka katika gereza la Bangwe ambako vitendo hivyo vimekithiri.
Hata hivyo, akijibu swali hilo Balozi Kagasheki alisema wizara yake imefuatilia kwa makini na kubaini hakuna jambo kama hilo, si kwa gereza hilo tu lakini, kwa nchi nzima kwa kuwa vitendo kama hivyo haviruhusiwi.
Alisema serikali haiwezi kutoa jibu la moja kwa moja juu ya adhabu zitakazotumika kuwaadhibu askari wa namna hiyo, kwa kuwa haijathibitika bado.
Aliitaja kanuni ya kudumu ya magereza ya mwaka 1968, kuwa haimruhusu askari kutothamini au kudharau ama kumdhalilisha mfungwa na kumtesa, huku akitaka ushahidi wa kutosha wa kuwaadhibu wahusika watakaobainika.
Hata hivyo, Sakaya aliitaka serikali kuachana na porojo za kutafuta nani awe shahidi na badala yake ushahidi mkubwa wa namna wanawake wanavyovuliwa nguo anao yeye mwenyewe.
Mbunge huyo alionekana kutoridhika na majibu ya Balozi Kagasheki wakati akijibu swali hilo la msingi ambalo alisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama wapo wanawake wanaoteswa na kudhalilishwa.
“Mheshimiwa spika, mimi ni shahidi namba moja katika jambo hilo maana nimekuwa ni miongoni mwa wahanga hao na jambo hilo lipo wanawake wanavuliwa nguo hadi ya mwisho na kubaki uchi wa mnyama waniulize mimi,’’ alisisitiza Sakaya na kusababisha wabunge kuangua kicheko.
Hata hivyo, baada ya ushuhuda huo wa Sakaya, Kagasheki alisema jeshi la magereza limekuwa likifanya upekuzi wa kawaida kwa ajili ya kujiridhisha kama vitu vya hatari haviingizwi ndani ya gereza.
“Kwanza nitoe pole kwa Mbunge Sakaya kama kutokana na kuvuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama, kama hilo lilimtokea basi tunasema pole sana, lakini upekuzi kwa jeshi ni kitu cha kawaida kwa ajili ya kuzuia vitu haramu visiingizwe,’’ alisema Kagasheki.
Jibu hilo la Kagasheki liliibua kicheko kikubwa ndani ya ukumbi huku kila mmoja wao akishindwa kujizuia na kumsababisha Sakaya naye aangue kicheko.Mwaka jana, mbunge huyo aliwahi kulalamika bungeni kwamba alifanyiwa vitendo vya kinyama akiwa rumande kiasi ambacho, na kuhoji kama yeye alifanyiwa hivyo wananchi wa kawaida wanatendea vipi kama si kupata mateso makubwa zaidi.
Kesi yake
Sakaya na wenzake hao wanashitakiwa kwa tuhuma hizo za kufanya mkutano bila kibali na kufanya uchochezi ambao ungeweza kusababisha vurugu na mbunge huyo alipofikishwa mbele Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Urambo, Oscar Burugu, lakini alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini kutoka mkoani humo wenye mali isiyohamishika na mwingine asaini hati ya mahakama ya thamani ya Sh3milioni.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Kiyungi Amri, Hashim Bakari, Yassin Mrutwa, Doyo Hassan ambao wote wanatoka nje ya mkoa wa Tabora, na wengine kutoka ndani ya mkoa wa Tabora ni Msafiri Kaidi, Mkiwa Juma, Singu Yusto, Mrisho Swedi, Chagu Salum, Zainab Saidi na Peter Charles ambao pia walirudishwa rumande.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Anthony Malisa, washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano ambayo yote yanahusiana na makosa ya uvunjifu wa amani.
Kwa pamoja wanadaiwa kufanya mkutano bila ya kuwana kibali, kumzuia ofisa wa polisi kufanya kazi yake, kujeruhi askari polisi waliokuwa kazini, kufanya jaribio la kupora silaha na kukataa kujitambulisha kwa askari waliokuwa kazini.

1 comment:
Isn't strip searching a standard prison procedure for processing inmates(men or women)for the first time?
Post a Comment