ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 17, 2012

VIONGOZI WA JUMUIYA NA WALIOGOMBEA UONGOZI, DMV WAKUTANA NA MHE. RAIS JAKAYA KIKWETE

 Kutoka kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Agnes Lusinde, Loveness Mamuya , Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Iddi Sandaly na Jacob Kinyemi wakiwa nje ya Hotel katikati ya Jiji la Washington, DC wakisubili kusalimiana na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambae yupo Nchini Marekani kwa mwaliko wa Rais Barack Obama ambayo pamoja na mambo mengine, atashiriki mkutano wa Nchi Nane Tajiri Duniani (G8) utakaofanyika Camp David na kuhutubia mkutano wa dunia kuhusu usalama wa chakula.  Rais Kikwete ni miongoni mwa marais wanne wa Afrika walioalikwa kwa ajili ya mkutano huo. Wengine ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Yayi Boni wa Benin, Rais John Mills wa Ghana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.
 Viongozi wa Jumuiya na Watanzania wengine waliogombea nafasi za uongozi, DMV wakijumuika pamoja na baadhi ya Wajumbe waliokuja na msafara wa Mhe. Rais kwa vitafunio na vinywaji laini Hotelini hapo.
 Juu na chini ni Viongozi wa Jumuiya na Watanzania waliogombea nafasi mbali mbali za uongozi DMV wakiwa na mmoja wa kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York, Shabani Mseba (kulia) waipata picha ya pamoja
 Mhe. Rais akiingia ukumbini huku akilakiwa na Mhe. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo, Chakula na Lishe
 Mhe. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kaimu Balozi Mhe. Lilian Munanka, kushoto kwa Mama Munanka ni Afisa Ubalozi Abbas Missana, Afisa Suleiman Saleh na Afisa Agnes Lusinde.
 Mhe. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Asia Dachi
 Aliyesimama ni Loveness Mamuya mmoja wa wagombea uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, akijitambulisha kwa Mhe. Rais, Dkt Jakaya Kikwete.
 Aliyesimama ni Aziz nae akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya kikwete
 Aliyesimama ni Shaban Mseba, kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania, New York nae akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.
 Aliyesimama ni muweka Hazina wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Ndugu Genes Malasy akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.
 Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Ndugu Iddi Sandaly akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete
 Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwananidi Maajar ( wapilli toka kulia) akiongea jambo baada ya utambulisho wa viongozi wa Jumuiya na baadhi ya wagombea waliogombea kinyang'anyiro cha uongozi, DMV kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

Kwa picha zaidi Bofya Read More

 

6 comments:

Anonymous said...

Bro, hebu pitia tena maelezo yako katika picha za Rais na viongozi wa DMV. Umeandika Rais wa DMV Iddi Sandaly akijitambulisha kwa Mhe Rais Iddi Sandaly....nadhani ilipaswa kuwa Mhe Rais Jakaya Kikwete.

Anonymous said...

niice....great team

Anonymous said...

wanajitambulisha nini wakati kikwete anawajua jamani.

Anonymous said...

Acheni wivu mnaacha kuwasifia mnajifanya kuwasahihisha,wabongo bwana sijui tutaendelea lini na kuacha chuki binafsi.

Anonymous said...

finally mambo yanaendeshwa kisomi....me like it!

Anonymous said...

Watanzania msipojisifia nani atawasifia ?kila kitu mnaponda hivi tutaendelea kweli ?mnavunja watu tamaa wivu haujengi bali unabomoa luka kazi nzuri sana unatuletea matokeo vizuri mungu akubariki na kazi yako isiyonamalipo