Advertisements

Friday, June 22, 2012

NSSF WESTADI KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU DOMITIAN RUTAHIMIRWA


Domitian Rutakyamirwa


Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) chini ya mpango wake wa WESTADI linatoa tamko kwamba litagharimia safari za kusafirisha mwili wa Ndg Domitian Rutahimirwa aliyefariki tarehe 18 katika Hospitali ya George Washington University, USA.

Kwa kuwa Marehemu alishajiandikisha katika Mpango wa WESTADI hivyo ni jukumu la Shirika chini ya mpango wake wa WESTADI kusafirisha mwili na kulipia gharama ya tiketi ya kwenda na kurudi  kwa mwanafamilia mmoja atayesindikiza mwili.

Tayari Uongozi wa WESTADI umeshafanya mawasiliano na Familia ya marehemu na utaratibu wa kulipia gharama hizo unaendelea.


Menejementi ya NSSF inatoa salam za rambirambi kwa wafiwa, ndugu na jamaa.



WESTADI NDIO TEGEMEO LA WANADIASPORA, JIUNGE SASA..



Kujiunga  na maelezo zaidi ingia hapa www.nssf.or.tz

3 comments:

Anonymous said...

ASANTE NSFF/WESTADI MNASTAHILI PONGEZI,WATANZANIA TUJIUNGE JAMANI.

Anonymous said...

Nivizuli sana kusikia hilo ila michango walitaka ya nini ya kusafirisha mwili kama Marehemu alishajiandikisha katika Mpango wa WESTADI.? kuna waliotoa michango hapo. NSSF ni mdhamini wa usafirishaji mwili nyumbani, nauliza tu michango itaendelea?

Anonymous said...

mbona tunaendelea kuchangishwa?????????????kana westadi wamedhamini sasa michango kwa nini inaendelea jamani watanzania mmezidisha.