Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28), jana alirudishwa mahabusu bila kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hadi hapo Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, itakapotoa uamuzi kuhusu suala la utata wa umri wake.
Baada ya mshtakiwa huyo kufikishwa mahakama hapo jana hakupandishwa kizimbani kutokana na jalada la kesi hiyo kuwa Mahakama Kuu, ambapo suala la utata wa umri wake litasikilizwa Juni 25, mwaka huu mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib.
Lulu alirudishwa mahabusu kutokana na sheria kutoruhusu usikilizwaji wa awali kuendelea wakati Mahakama Kuu inaendelea kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na mshtakiwa kutaka umri wake uchunguzwe.
Katika kesi hiyo, Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment