ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 2, 2012

Mwambene awa Mkurugenzi Maelezo

Idara ya Habari Maelezo  imepata Mkurugenzi mpya ambae ni Asah Andrew Mwambene (41).

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana, ilisema Mwambene aliteliwa tangu Julai Mosi mwaka huu na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambae mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Mwambene kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha Mwambene amewahi kufanya kazi katika kampuni ya magazeti ya serikali (TSN)  akiwa mwakilishi wa kampuni hiyo huko Zanzibar.

No comments: