Muogeleaji Magdalena Moshi
Muogeleaji mwingine wa Tanzania, Magdalena Moshi, ameaga mashindano ya kuogelea ya Michezo ya Olimpiki baada ya kutolewa katika hatua ya kwanza ya michuano ya mita 100 'freesytle' jijini London, Uingereza jana.
Magdalena amekuwa Mtanzania wa tatu kutolewa baada ya bondia Seleman Kidunda kudundwa kirahisi katika hatua ya kwanza, na muogeleaji wa kiume Ammar Ghadiyal kutolewa katika hatua ya kwanza pia juzi.
Akizungumza na NIPASHE jana, mkurugenzi wa ufundi wa chama cha kuogelea nchini (TSA), Marcelino Ngalioma, alisema Magdalena alishindwa katika mchujo wa awali.
Magdalena, kama Ghadiyal, naye alikuwa akiogelea kwa kujifurahisha kutokana na kuingia katika michuano hiyo kwa nafasi maalum za upendeleo kwa vile hawakufuzu hivyo hata kama angeshinda asingepewa medali.
Matumaini ya Tanzania yamebaki kwa wanariadha wake wanne ambao wataanza kutupa karata zao Agosti 8 ambapo Zakia Mrisho atachuana kuwania medali katika mbio za mita 5,000.
Atafuatiwa wanariadha Samson Ramadhan, Mohamed Msenduki na Faustine Mussa ambao watawania medali za mbio za marathon Agosti 12.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment