Advertisements

Friday, August 31, 2012

SHUKURANI


P.O.BOX 56356 WASHINGTON DC 20040
TEl# 240-4230437 202-629-7841 Email address:ccmwashdc@gmail.com

31 August,  2012


 SHUKURANI KWA WANA CCM DMV

Chama Cha Mapinduzi kinatoa shukurani za dhati kwa wanachama wake waishio maeneo ya Washington, DC , Maryland na Virginia kwa mchango wao wa hali na mali walioutoa katika kufanikisha sherehe hizi za ufunguzi wa Tawi.
Kwa kweli uongozi wa tawi umefarijika sana kuona wanachama wengi waliweza kuhudhuria sherehe hizo za ufunguzi wa tawi lao. Vile vile, sura hii imeonyesha namna gani chama cha mapinduzi ni chama bora kinachoweza kuwaunganisha wanachama wake popote duniani ili waweze kujiusisha na siasa ndani ya nchi yao. Hii ni fursa nyingine itakayowawezesha wanachama wa CCM kuchangia maoni bora yatakayowezesha kuimarisha chama na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi wa nchi yao. Tunawasisitizia watanzania CCM ni chama tawala ambacho kina penda amani na utulivu sio chama cha vurugu na tunawahakikishia wanachama wote wa ccm muishi na watanzania wengine kwa upendo, amani na utulivu na kuweza kushirikaana na watanzania wenzetu katika mambo ya kila siku bila kujali tofauti za kisiasa. Sisi sote ni watanzania. Wana CCM tuwe mfano bora kwa jamii.

Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:

1. Binadamu wake ni sawa bila kujali rangi, dini, kabila au maeneo aliyotokea mwanachama wake.
2. Kila mwananchi anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Kumshirikisha mwanachama kuchangia maoni yake ili kuimarisha sera na utekelezaji katika chama chake.

Amani , Upendo, Uzalendo na utaifa ni msisitizo mkubwa wa chama cha Mapinduzi kwa mtanzania popote alipo duniani. Sera hizi za CCM zimeifanya Tanzania kuwa kisiwa cha Amani na Utulivu barani Afrika.

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA  NA TUNASONGA MBELE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ASANTENI SANA
Imetolewa na mwenyekiti wa tawi-DMV- Marekani
loveness Mamuya

No comments: