Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa
Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali
inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo
kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika
hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia ni
Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo
hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora
za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi
Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba
alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais
wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Na Francis Godwin iringa
No comments:
Post a Comment