Thursday, December 27, 2012

SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE LAVIUS KALEMERA

Familia ya Marehemu Lavius Kalemera inapenda kutoa shukrani nyingi sana kwa watanzania wote na rafiki wote waishio Marekani, kwa kuweza kumuuguza mzee Kalemera kwa muda mfupi aliougua, wote mlikuwepo kwa hali na mali. Pia baada ya Mwenyezi kumuita pia mlikuwepo bega kwa bega na kuwezesha mwili wa marehemu unasitiriwa na kusafirishwa. Mwili wa marehemu utasafirishwa leo tarehe 27/12/12 saa 10.25.mchana kwa ndege ya KLM na kuwasili Dar Ijumaa tarehe 28/12/12 saa 4.40 usiku. Baada ya hapo mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea Kanazi Kagera Jumamosi tarehe 29/12/12 na mazishi yatafanyika Jumatatu tarehe 30/12/12. Familia inasema haina malipo ya kuweza kutoa kwa mchango wenu watanzania ila inaomba Mwenyezimungu awape malipo yanayo stahili kwa wote. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi.

No comments: