Advertisements

Friday, December 7, 2012

SIRI YA MTUNGI YAONYESHA NGUVU ZA SEKTA YA SANAA

MFDI Tanzania ndio watunzi wakuu wa thamthilia mpya ya kusisimua Siri ya Mtungi. Mkurugenzi wa MFDI Tanzania, John Riber, katika muda wote wa maisha yake ya kutengeneza filamu, kuanzia India na Bangladesh had Zimbabwe na Tanzania, hajawahi kupata uzoefu kama huu.


Kwa Riber, tamthilia hii imemruhusu kuunganisha uchawi wa filamu na mahitaji ya maendeleo na nguvu ya elimu. Alisema Bw. Riber kwamba sanaa ya uigizaji kwa ujumla inaweza kuinuia uchumi wa nchi nzima. Inaguvu ya kuajiri na kunufaisha jamii kwa mfano, huko Nigeria sanaa na filamu in ajiri asilimia kubwa ya watu zaidi ya biashara na taasisi zingine ispokuwa serikali ya nchi hiyo.

“Niligundua mapema katika kazi yangu hii kuwa nilichokihitaji kukifanya hasa ilikuwa kutumia nguvu ya filamu kuingilia moja kwa moja mchakato wa maendeleo au mageuzi ya kijamii. Nilitaka kutumia filamu kwa watazamaji kwenye nchi zinazoendelea, kutayarisha filamu kwa maendeleo, kinyume na utengenezaji wa filamu kuhusu maendeleo. Na hivyo ndivyo tunavyokabili kazi zetu zote hapa MFDI.”
SIRI YA MTUNGI AND THE CREATIVE FORCE BEHIND IT (ENGLISH)

MFDI is the creative force behind New TV series Siri ya Mtungi. MFDI Country Director, John Riber, has not experienced anything like it in his long career making films and dramas, from India and Bangladesh to Zimbabwe and Tanzania.

For Riber, the series has allowed him to combine the magic of film together with the necessity of development and the power of education as well as the ability to develop capacity and employment in Tanzania. For example, he states that the Nigerian film industry is the second largest employer in the country behind the government.

“I discovered early in my career that what I really wanted to do was to harness the power of film as a direct intervention in the process of development or social transformation. I wanted to use film for audiences in developing countries, making films FOR Development, as opposed to making films ABOUT Development. And that is how we approach our all work at MFDI.”

No comments: