ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 12, 2012

VIDEO YA SIKU RAY C ALIPOFIKA IKULU KUMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA MATIBABU


Siku mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila, maarufu kama RAY C, alipomtembela Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Desemba 10, 2012 Ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliyompatia wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni. Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake sasa imeimarika na kwamba muda si mrefu ujao atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

1 comment:

Anonymous said...

Kaka Luka, naomba ni kushare na wengine hii clip ya Hurricane Sandy....touching story and pictures hasa hizo sanamu....

http://screen.yahoo.com/weekly-flickr-hurricane-sandy-202806964.html