Askofu Dkt Mdegela
Na .Said Ng'amilo Iringa.
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi
yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu
uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na
uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa
vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa
mpango huo.
Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa
ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi
hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati
huo.
Kufuatia hali hiyo, Mdegela amewaandikia waraka, wanachama wote
waJumuiya ya Makanisa ya Kikristo nchini (CCT) kuanza mara moja
mfungowa saa 24 kuanzia leo (Maombi ya mnyororo), kusali dhidi ya
uhalifuhuo kwa minajili ya kuwasaidia makachero kutoka ndani na nje ya
nchikuwabaini wanaotekeleza mkakatihuo.
Dk. Mdegela alitoboa siri hiyo wakati akizungumza na Waaandishi wa
Habari katika kanisa kuu la kkkt lililopo eneo la Miyomboni sokoni
”Vikundi hivyo vinataka kuichafua serikali,kuuvunja muungano na
kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kidini. Serikali ichukue au isichukue
hatua, sisi tunakwenda madhabahuni na ndio maana nimeitisha maombi kwa
makanisa yote ambayo ni wanachama wa CCT,
...Ingawa matamko haya, hayawezi kumaliza tatizo isipokuwa tutasugua
goti ili kudhihirisha nguvu ya maombi,”Alisema Mdegela aliyekuwa
ameongozana na wachungaji na baadhi ya wakuu wa majimbo ya KKKT.
Kuhusu usalama wa makanisa yaliyopo chini ya KKKT na CCT, Askofu
Mdegela ameagiza kila kanisa liimarishe ulinzi kila kona kutokana na
mkakati unaotekelezwa kwa kificho na vikundi vinavyoshukiwa.
”Naagiza wekeni ulinzi kuanzia geti la mbele, la nyuma na kwenye
kengele ili wakitokea watu hao, walinzi wapige kengele na kupambana
nao. Huu ni wakati wa wakristo wote nchini kuingia na kuzama katika
maombi ya mnyonyoro kuomba amani na kuepusha vurugu za kidini
zinazoendelea nchini hivi sasa,”Alionya askofu huyo.
Alifafanua kuwa vurugu hizo, zinatokana na baadhi ya vikundi vya
kidini ambavyo amedai kwamba vinafadhiliwa na nchi zenye msimamo mkali
kutaka kuueneza dini mojawapo kwa nguvu bila kufuata utaratibu na
sheria za uenezaji.
Askofu Mdegela amewataka wakristo kwa muda uliopo kuutumia katika
maombi na kutojiingiza katika kuonesha tofauti za ukristo bali ni
wakati wa kuungana kwa pamoja na kuingia katika maombi kwa kipindi
chote kwa ajili ya amani na utulivu.
Aliyataja matukio ya kuuawa kwa Mchungaji wa Kanisa wa kanisa la
kiroho katika mkoa mpya wa Geita,kuuawa kwa Padri Evarist
Mushi,kushambuliwa kwa risasi mwilini kwa Paroko Ambrose Mkenda,uchomaji
moto nyumba za ibada na uharibifu wa mali za makanisa kadhaa nchini ni
matokeo ya mkakati huo.
"Kanisa limeingia katika mateso na tumesema hatutalipiza isipokuwa
tunakwenda madhabahuni na kupiga tukiomba maombi ya mnyororo na
tutashinda,"Alisisitiza Mdegela.
wanataka nchiyetu isitawalike tuwekama nchi zisizo na amani duniani.
Tunaimani umojaninguvu utenganoniudhaifu.
2 comments:
Pamoja na mawazo mazuri ya askofu. Nafikiri tufanye tamasha kubwa la nyimbo za Injili kuwaonyesha kwamba WATASHINDWA IN JESUS NAME!!!
mchochezi sana huyu askofu dkt mdegela toka zamani tunamjua kuna kitu wanakipika lakini mungu atawaubua na njama zao zimeshajulikana yeye si mungu wala dini yake si ya mungu.
wangalieni jinsi wanavyo suka plan zao hawatoweza katu kukikidimiza kisiwa cha zanzibar na pemba kwa idhni ya rahman AMIN AMIN AMIN
Post a Comment