ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 19, 2013

DARASA LA KISWAHILI KWA WATOTO DMV- KUANZA WIKI HII

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV
Darasa la Kiswahili Kwa Watoto

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV unapenda kuwajulisha watanzania wote wa DMV kuwa, tutakuwa na Darasa la Kiswahili kwa Watoto wetu wa hapa DMV kuanzia Tarehe 23, Mwezi wa Tatu. (March 23, 2013). Darasa hili litafanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi na nusu za Jioni.(4:30PM). Anuani ya Darasani ni:
3621 Campus Drive, College Park, MD

Kwa Kujiandikisha Tunaomba utume jina Kamili la Mtoto na Mawasiliano ya Mzazi au mlezi (kipeperushi na namba ya simu), kwenda: info@watanzaniadmv.org au piga simu 240-645-2131 au 301-793-2833.


Wenu
Uongozi.
Jumuiya ya Watanzania DMV

2 comments:

Anonymous said...

je Mwalimu ni nani?Mbona aweki details zake

Anonymous said...

Simu huzioni hapo? Au wewe kipofu? Kama una swali wapigie iliwakujibu. Au ndio nyie msio sikia la Muazini wala la mnadi swala?