ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 18, 2013

TRAFIKI AGONGWA NA GARI ENEO LA BAMAGA

Trafiki wa kike aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.
Hali ilivyokuwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.
Baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.

Trafiki mmoja ambaye amefahamika kwa jina moja la Elikiza, muda huu amegongwa na gari aina ya VX ambayo haikujulikana namba na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo wakati akiongoza magari eneo la mataa ya Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa Trafiki huyo alikuwa akiongoza msafara na baada ya msafara huo, aliruhusu magari mengine yaendelee na safari ndipo ghafla gari lilipotoka upande wa pili na kumgonga.

(Picha na Shauri Kati / GPL)
Kwa picha nyingine kwenye read more na tunaomba radhi kwa picha hiyo


Trafiki Elikiza baada ya kugongwa na gari eneo la Bamaga muda huu.


1 comment:

Anonymous said...

Hivi hao waendeshaji wa magari wanavuta bangi? Ni lini huko Tanzania watu watafuata sheria na taratibu za kuendesha magari? Na kwanini watu wanakimbia baada ya ajali? Ni kwa nini mtu aliyejeruhiwa anakaa muda mrefu kabla ya ambulance kufika? na hakuna CPR, sasa nani amethibitisha kuwa amefariki? kuna hatari watu wanakuwa pronounced dead wakati bado wazima.