Leo Waendesha Daladala au Vifodi jijini Arusha Mjini wamegoma kuishinikiza Halimashauri ya jiji ya Arusha mjini kuweka vituo vinavyoeleweka kutokana na kusumbuliwa mara kwa mara na matrafiki wa jiji la Arusha.
Madereva waliogoma ni kwa upande wa Njiro,Kijenge,Mbauda,Majengo,Sombetini na sehemu mbalimbali za Arusha Mjini.
Mwandishi wetu alifanya maojiano na baadhi ya madereva wa daladala wamesema wamechoshwa na kamatakamata ya hapa na pale.
Pia wameishutumu Uongozi wa jiji la Arusha kuuza vituo vya mwanzo vya kushusha na kupandisha abilia walivyokuwa wanatumia kwa kipindi cha mwanzo kwa wahindi kuwa paking zao.
No comments:
Post a Comment