Advertisements

Tuesday, April 9, 2013

MAALIM SEIF AUNGURUMA KIKWAJUNI

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar naKatibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akiwahutubia wananchi wa Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho uliofanyaka katika viwanja vya mpira Mkwajuni, April 06/2013
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akiwahutubia wananchi wa Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho uliofanyaka katika viwanja vya mpira Mkwajuni, April 06/2013
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akisikiza utenzi kwa makini,kulia ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Hamad Masoud Hamad na kushoto Mwenyekiti wa Wilaya ya Kaskazini (A). huko Mkwajuni Kaskazini A Unguja.
Wanachama wa CUF wakisikiliza kwa makini Maalim Seif Sharif Hamadi hayupo pichani alipokuwa akiwahutubi katika mkutano wa hazara uliofanyika katika viwanja vya mpira Mkwajuni.

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar ni nchi ya biashara hivyo inataka kujitegemea iweze kupunguza ushuru ili wananchi wapate kununua bidhaa kwa bei nafuu.

Kauli hiyo ameitoa huko katika viwanja vya Skuli ya Mkwajuni Wilaya ya kaskazini “A” wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa huo.

Amesema iwapo Zanzibar itapata mamlaka yake kamili itaweza kuwa na bandari huru, ushuru na bei za bidha vitapungua.

“Zanzibar ni nchi ya biashara tunataka tuwe na bandari huru ili tupate kuweka kodi ndogo na ushuru ukipungua bei za bidhaa zitapungua”alieleza Maalim.

Aidha amesema kuwa wananchi wanataka kuwepo kwa bandari na kupungua ushuru ili wapate kuweka bei wanazotaka wenyewe na sio kuamuliwa na mtu mwengine.

Akizungumzia Muungano Maalim Seif amesema wazanzibari waliowengi wanataka serikali ya mkataba iwe na mamlaka kamili na isiingiliwe katika maamuzi yake.

“Haya ni matakwa ya wananchi wenyewe na sio matakwa ya CUF hili ni la wazanzibar wenyewe” alieleza Katibu huyo.

“Zanzibar ni nchi matakwa ya wazanzibari yaheshimiwe yasiingiliwe na wengine kwani mamlaka na madaraka hayo ndiyo yanayoweza kuyatatua matatizo ya wazanzibar” alifafanua Maalim Seif.

Hata hivyo Katibu huyo ameitaka Tume ya kukusanya maoni ya Katiba kuhakikisha kwamba wajumbe waliochaguliwa kuwakilisha kutoa maoni katika Katiba hiyo wamechaguliwa kihalali na sio kupandikizwa.

IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI MAELEZO- ZANZIBAR.

No comments: