Mbunge wa Jimbo la
Nzega, Dr. Hamis Kingwallah
Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.
Nawasalimu kwa heshima na taadhima.
Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa wanahabari na
umma kwa ujumla kufuatia habari iliyotoka leo mapema asubuhi kwenye gazeti la
Sauti ya watu Tanzania Daima, toleo Na.3071 na kuzua mjadala mkubwa na mzito
kwenye jamii pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hadhi, heshima
na uadilifu wangu kwenye jamii nikiwa kama kiongozi wa umma. Niwape pole wale
wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili, haswa familia yangu, ndugu,
marafiki na wananchi wa Nzega; ambao siku zote wanaamini sana katika uadilifu
wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.
Nimesikitishwa sana na habari hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila kunipa
fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na
kueleza upande wangu wa hadithi.
Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kwenye baadhi ya
vyombo vya habari kuandika habari za uongo kwa maslahi maovu ya kuwachafua
wanasiasa na watu wengine. Watanzania sote tubadilike na tukatae tabia za
kutumika vibaya namna hii, maana ni hatari kwa ustawi wa weledi, na kwa umoja
na mshkamano wa kitaifa. Ukishaandika jambo ambalo litamchafua mwenziyo, hata
kama utamsafisha kiasi gani ni wazi hautokuwa na uhakika kuwa utawafikia wale
wale waliosoma zile za jana za kumchafua – hivyo ni jambo la kawaida kabisa
kuanza kwanza kwa kuwa na uhakika kabisa na habari kabla ya kuiandika.
Mfano mwaka 2010 tu mara baada ya kuteuliwa nilizushiwa
kashfa ya uongo kabisa inayohusiana na Uraia wangu na gazeti moja maarufu la
kila siku na mengine yakaweka kwenye ukurasa wa mbele kabisa kwamba Kigwangalla ni Mrundi; hawakusema ni
mrundi wa wapi, toka lini ama kivipi, walisema ni mrundi tu! Basi hata kusema
shaka yao inaanzia wapi hawakusema. Kwa kuwa vyombo vya dola vilinisafisha na
kupelekea kushinda mapingamizi yote yaliyowekwa na washindani wangu kisiasa,
niliamua kudharau na kusema yatapita tu na yatasahaulika.
Pia gazeti lingine likaandika kwamba kampuni ya Kigwangalla
ni miongoni mwa makampuni yaliyowahi kufaidika na ‘stimulus package’ baada ya
mdororo wa uchumi mwaka 2008. Gazeti hata halikutaja kampuni ya Kigwangalla ni
ipi, inaitwaje, Kigwangalla ana hisa kiasi gani, anaendesha kampuni hiyo ama
la, na kampuni hiyo imepewa sh ngapi kutoka benki kuu, na je imepewa pesa hizo
kwa nyaraka zipi na zenye namba gani? Na je pesa hizo imepewa kihalali ama imepitia
mlango wa nyuma? Kama imezipata pesa hizo kinyume na utaratibu, basi kuna
ushahidi gani! Kwa kuwa yalikuwa mambo ya uongo na uzushi niliamua kudharau na
kuacha kama ilivyo.
Gazeti lingine la kila siku liliwahi tena kuandika
‘Kigwangalla atajwa kufadhili mgomo wa madaktari’ na liliweka hadithi hii
kwenye ukurasa wake wa mbele kabisa. Halikusema amefadhili sh ngapi? Amempa
nani? Zimeenda kufanya nini fedha hizo? Kwa kuwa lilikuwa ni jambo la uongo,
pia nilidharau na kuacha lipite. Mwaka jana Novemba pia gazeti lingine
liliandika habari na kuweka picha yangu na ya Ndg. Hussein Bashe, na katikati
yetu picha ya bastola, na kusema ‘Kigwangalla na Bashe na vita ya bastola
Nzega’, na humo ndani kueleza kuwa Kigwangalla na Bashe wanyoosheana bastola
wakati wakirudisha fomu za kugombea ujumbe wa NEC. Na kuna mengine mengi: yale
ya rushwa ya vitumbua n.k.
Yote haya kwa ujumla
wake yalikuwa ni mambo ya uongo na yasiyo na chembe ya ukweli hata kidogo. Mara
zote nimekuwa nikiyadharau na kuongea na
wahariri wa vyombo husika vya habari kwa namna inayoashiria urafiki na weledi wa
kushirikiana na kufanya kazi pamoja na si vinginevyo; ushauri ambao
niliupata mwaka 2009 kutoka kwa moja ya wanasheria wa kampuni yangu (wa kampuni
ya Marando, Mnyele & Co. Advocates), wakili nguli Mzee Mabere Nyaucho Marando, ambaye alisema ‘wasamehe tu hawa gazeti la
Sauti Huru maana ni vema kujenga marafiki wengi zaidi na media kwa kuwa wewe ni
kijana, kuliko kujenga maadui – na niliwasamehe bila gharama yoyote ile’. Mzee
Marando hakukosea, ila ukweli ni kwamba ukifanya hivyo utaona patatulia kwa
muda na baada ya hapo pataibuka tena jambo lingine la ukurasa wa mbele
linaloandikwa bila ukweli wowote ule! Imekuwa wimbo wa kawaida kwenye baadhi ya
media houses! Kufanya kazi kwa maslahi ya watu fulani ama chama fulani, misingi
ya weledi ya uandishi haipo! Cha muhimu ni maelekezo ama utashi wa anayetoa
chochote.
Jambo moja kubwa nililojifunza kutokana na yote haya ni
kwamba, jambo likiishaandikwa kwenye media halifutiki kwenye bongo za watu,
hata muda ukipita namna gani! Leo hii kila siku haya mambo yamekuwa yakirudiwa
rudiwa kwenye mitandao ya kijamii hata baada ya kuyatolea ufafanuzi wa kina.
Nimefika mahali nimeona niachane na passive ways za kushughulika na media ili
kuweka sawa kumbukumbu zangu mbele ya umma wa watanzania.
Ya ukweli: ni
kweli kwamba ninamiliki hisa kwenye kampuni ya Emergent Africa Ltd. Nina hisa 40% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla
anamiliki hisa 11%. Sijihusishi na kuendesha biashara hii kama mtendaji wa
kila siku – kampuni ina watumishi wake sehemu mbalimbali. Ni kweli kwamba
kampuni ina mradi wa kujenga chuo cha afya Nzega (International Institute for
Health Tabora), eneo la uchama, na ni kweli imepewa orodha ndefu ya vitu
ilivyosamehewa kodi na serikali kwa kuwa ni vitu/vifaa vya mtaji (deemed
capital goods). Ni kweli kwamba kampuni imewahi kuingiza nchini kontena moja
lenye vifaa vichache sana katika vinavyotajwa kwenye habari ile, na vingi kati ya hivyo vipo aidha kwenye stoo
ya kampuni iliyopo Nzega ama ya Dar es salaam, Kigamboni. Kwa kuwa vipo,
wanahabari wanakaribishwa kwenda kuvitazama vitu hivi kama wanapenda.
Ya uongo: Si kweli
kwamba nina hisa 78% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla ana hisa 22% - ni
uongo. Si kweli kwamba kampuni imeagiza
vitu na kuvipitisha bandarini na forodhani kwa msamaha kwa nia ya kuuza na
hivyo kuiibia serikali kwa njia ya kukwepa kodi. Si kweli kwamba kampuni ya Emergent Africa Ltd imeingiza vifaa vyote
ambavyo imepewa msamaha, kama habari inavyotaka kuwaaminisha waTanzania.
Sijawahi kuuza bidhaa zozote zile za kampuni hii zilizoingizwa nchini kwa njia
ya msamaha wa kodi. Kampuni ya Emergent Africa Ltd haina mradi wa kuuza tiles
na hivyo haijawahi kufanya biashara hiyo.
Ingekuwa ni dhambi kubwa kama kweli ningekuwa naviuza vifaa
hivi bila kuvilipia kodi. Na kama ningekuwa sina mradi genuine wa ujenzi wa
chuo na labda nimetumia vibaya nafasi yangu ya ubunge kujipatia msamaha ili
kurahisisha biashara zangu basi ningeanza
kwa kuuza cement (ambayo ni bidhaa inayokimbia sana sokoni na kampuni yangu
imepewa msamaha wa karibu tani 5000 – lakini sijawahi kuutumia msamaha huu
kununua hata mfuko mmoja wa cement!). Ama ningeingiza mabati/vigae vya kuezekea
(ambavyo pia vinakimbia sana sokoni kwa kuwa watu wengi wanajenga – lakini
sijaingiza hata kigae kimoja!), ama ningeingiza malori 4, Nissan Navara pick up 4, Mitsubishi Canter 2, Landcruiser
Hardtop 4( ambazo zinatumika sana kwenye utalii na hata kwenye barabara za
vumbi) kwa msamaha – lakini sijaingiza hata gari moja kati ya haya, kinyume na
habari hii ya Tanzania Daima inavyotaka kuuaminisha umma! Kuonesha uadilifu nitaeleza hapa mfano mmoja kwamba mnamo Novemba
mwaka jana nilinunua gari moja SUV aina
ya Nissan Patrol (T934 CDB) na nimeilipia kodi zote bila msamaha japokuwa
ningeweza kutumia msamaha wa kodi kununua na kuingiza moja ya magari yaliyopo
kwenye msamaha huu wa kampuni ambayo mimi ni major shareholder. Pia nina ujenzi
wa nyumba ya kuishi Nzega, Tabora na Dar es salaam katika hatua mbalimbali:
ningeweza kutumia msamaha huu wa kodi wa kampuni yangu ili kujipatia unafuu
kwenye manunuzi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi kama cement, vigae ama mabati,
lakini sijawahi kufanya hivyo hata siku moja!
Kuwa na hisa kwenye kampuni inayofanya biashara halali siyo
dhambi. Kupata msamaha wa kodi siyo dhambi. Dhambi ingekuwa kuviuza baada ya
kupata msamaha. Kama kuna mtu anaamini kuwa kuna vifaa vimeuzwa na kampuni
yangu, kati ya hivi vilivyoingizwa nchini kwa msamaha, anakaribishwa kuleta
uthibitisho wa nyaraka za mauzo (cash
sale receipts, tax invoice ya mauzo, pay-in slip ya benki ya malipo, delivery
note, ama receipt yoyote ile ya kampuni hii inayoashiria kuwa mauzo
yamefanyika) ili niweze kufuatilia kujua ni nani aliyeuza na kwa nini alifanya
hivyo ili niweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake ikiwa ni pamoja na
kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria.
Msamaha wa vifaa hivi ni kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha Afya Nzega (kitakachoitwa
International Institute for Health Tabora), ambacho nilikianza kwa fedha zangu mpaka
pale kilipofikia na sasa tunasubiria majibu ya benki ya maombi yetu ya mkopo
ndipo tuendelee. Na msamaha huo upo na hautotumika kwa mambo mengine ya binafsi
kama nilivyoeleza hapo juu kwenye ununuzi wa gari langu binafsi la kutembelea
na ujenzi wa nyumba yangu binafsi ya kuishi Nzega, Tabora ama Dar es salaam
(ambako ninajenga).
Watanzania tuache kushabikia uongo. Kufanya hivyo kunaziba
mianya ya ukweli kutamalaki. Tuache kutazama mambo kwa macho ya wivu, husda na
majungu. Tusimame kwenye misingi ya ukweli daima. Nchi hii itaendelezwa na watu
wenye kuchukua maamuzi thabiti na hatua za maksudi za kuleta mabadiliko – kama
miradi ya namna hii (ya chuo cha afya Nzega kule!). Nchi yetu bado ina watu
waaminifu na waadilifu na tunaamini tutafanikiwa kuwadhibiti walio waovu. Hata
siku moja kweli haijawahi kushindwa vita na uongo. Si kila mtu aliyeko kwenye
uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi wapo pia. Tusimuangalie
kila mtu kwa sura ya ‘ufisadi’ na ‘ubadhirifu’ tu! Tuaminiane jamani.
Tusifedheheshane na kukatishana tamaa. Safari kuelekea mapinduzi ya maisha ya
watanzania kiuchumi na kijamii bado ni ndefu lakini tutafika. Tufanyeni kazi.
Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi
mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla, M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu
ya kiganjani ni 0782636963 na email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )
Hii chini ni taarifa iliyoandikwa na Tanzania Daima
UFISADI WA DR KIGWANGALLAH
MBUNGE wa Nzega, Dk.Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia taifa
kwa kutumia vibayamisamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili
ya ujenzi wa chuo cha afyaeneo la Uchama, wilaya ya Nzega.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, Dk.
Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko lathamani na
ushuru wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited,
anayoimilikikwa asilimia 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22.
Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchinibidhaa mbalimbali
ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka lakuuza
vifaa vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine
anaziuza kwawafanyabiashara wengine.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni yaEmergent Africa Ltd,
ilisajiliwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC)Septemba 27,
2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011hadi
Agosti 2014.
Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni yaEmergent Afica Ltd na TIC,
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehekodi kampuni hiyo
ya Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba1 hadi
390.
Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042,mashine za kutolea kopi 12,
printa 12, ‘binding machines’ 12, vikokotozi(calculator) 640, projekta
12, video kamera 12, feni 30, vifaa vya simumasanduku 28, jenereta
moja, magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan NavarraPik up 4,
Mitsubishi Canter 2 na mabasi madogo manane.
Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallahkupitia kampuni hiyo, aliingiza
nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigaevya sakafuni 2500 vyenye
ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400pamoja na vigae
vya ukutani.
Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia,hema la bustanini, sofa,
kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro,televisheni na
vingine.
Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada yakupokea bidhaa hizo kutoka
nchini China, ziliuzwa katika madukambalimbali ya Kariakoo na vigae
vingine kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoaniTanga (hatukumtaja) kwa
kuwa hakupatikana kujitetea.
Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakarahizo kwani kampuni ya
Delmas iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk.Kigwangallah,
ziko tofauti na ankaraza malipo.
Ankarahizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino
Investment andDevelopment Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan
na Sharpeye Furniture.
Wakati manunuzi yakionekana kufanyika ChinaOktoba mosi, 2012, nyaraka
nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tanguAprili 14
mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN100-145-596,
risiti namba 2012/0000002986.
Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyeshabidhaa hizo ziliingia
nchini Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishanakatika tarehe
za kununua na kuingiza bidhaa hizo.
Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa zaShirika la Viwango
Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwaMachi 28,
2012.
Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana zamakampuni mawili ya
kibiashara wakati ankaraya malipo ilikuwa moja.
Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini
lilionekana kuwa na vitu tofauti navile vilivyoorodheshwa, hivyo
kusababisha kontena hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida
kwakupekua mzigo mmoja mmoja.
Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simukufafanua tuhuma hizo, alisema
amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwamaswali kwenye barua pepe
yake, aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.
Alipopigiwa tena jioni, alisema, “Sema harakaunataka nini?”
Alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikata simu.
Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu:“Nitakupigia jioni nikitoka bungeni.”
Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini,alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa
tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua

No comments:
Post a Comment