Advertisements

Tuesday, July 9, 2013

UBALOZI WASHINGTON, DC WAMUAGA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI

Juu na chini ni Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongea machache katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani katika kumuaga baada ya kumaliza ziara ya siku tano aliyofanya Washington, DC na kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani lililofanyika Jumamosi July 6, 2013 Capitol Heights, Maryland.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiingia Ubalozini kwenye chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi huo kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano.
Juu na chini ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC wakiwemo wanakamati wa miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani/
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Sitti Mwinyi (watatu toka kulia) wachukua chakula walichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani walipoandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwaaga.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitambulisha wakati mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye chakula hicho na kumtakia safari njema .
Mwenyekiti wa Kamati, Bwn. Baraka Daudi akijitambulisha kwa mgeni rasmi na kumtakia safari njema nyumbani.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika picha ya pamoja na Maafisa wakiwemo wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani.
kwa picha zaidi bofya read more




No comments: