Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. John Samuel Malecela akisisitiza jambo wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na Baadhi ya maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ( hawapo pichani) na wajumbe wanaohudhuria mikutano ya Kamati Kuu Sita za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mhe. Malecela ambaye yuko Jijiji New York kwa ziara binafsi akifuatana na Mkewe Mhe. Ann Kilango, alisisitiza sana umuhimu wa watanzania wote bila ya kujali itikadi na tofauti za kisiasa, kuhakikisha wanaulinda mtaji wao mkubwa ambao ni amani.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Mkewe Upendo wakifuatilia mazungumzo hayo ambayo yalifanyika katika makazi ya Balozi , mazungumzo yaliyoambatana na chakula cha jioni.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwa na maafisa wengine wakimsikiliza Mhe. Malecele
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Upendo na Bi. Tuusume
Afisa Mambo ya Nje, Bi Ramla akiwa na mmoja wa wajumbe wanaohudhuria mikutano inayoendelea katika Umoja wa Mataifa
Chakula cha jioni kikiendelea kuliwa
Na Mwandishi Maalum
Waziri Mkuu mstaafu
Mhe. John Samue Malecela ameeleza kwamba, hakuna mtaji mkubwa ambao watanzania wanauhitaji kama
amani.
Ameyasema hayo
mwishoni mwa wiki wakati alipokutana
na kubadilishana mawazo na
maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, pamoja na wajumbe wanaohudhuria
mikutano inayoendelea ya Kamati Kuu Sita za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mazungumzo hayo
yaliyoambatana na chakula cha jioni yalifanyika
katika Makazi ya Muwakilishi wa Kudumu
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
“ Naomba niliseme
hili, ninasema hivi , hakuna mtaji
mkubwa tunaouhitaji watanzania wote bila
ya kujali itikadi wala tofauti zetu za kisiasa
kama amani” akasema Mhe. Malecela .
Na kuongeza. “Nchi
yetu inaoutajiri usioelezeka, hakuna
wilaya isiyokuwa na utajiri kuanzia gesi, madini ya kila aina, ikiwani
madini ya namna ya urani hadi makaa ya mawe, nchi yetu ni tajiri sana.
Tunahitaji mitaji ya kuendeleza utajiri
huu. Lakini nasisitiza sana utajiri huu
tulionao hautakuwa na maana yoyote kwetu watanzania kama hatutadumisha amani,
upendo, mshikamano na uzalendo”.
Waziri Mkuu mstaafu
na ambaye amefuata na mkewe Mama Ann Kilango yupo jijini New York kwa ziara binafsi.
Akasema uchimbaji wa
gesi ukianza na uchimbaji wa madini ya urani ukianza, pamoja na mipango
mbalimbali ya maendeleo inayoendelea hivi sasa, basi miaka kumi ijayo Tanzania itapiga hatua
kubwa sana za kiuchumi na kimaendeleo.
Katika mazungumzo
hayo Mhe. Malecela licha ya kuzungumzia
umuhimu wa amani na matumizi mazuri ya
raslimali , pia alizungumzia mafanikio
na changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa hivi sasa.
Kwa upande wa
maendeleo hakusita kuzungumzia mpango wa
serikali wa kuwa na shule za sekondari kila kata na kusisitiza kwamba
ingawa uamuzi huo umekuwa ukipingwa au kulalamikiwa na baadhi ya watu lakini ni
mpango ambazo umewapatia fursa vijana wengi ya kupata elimu ya sekondari na matunda yake yanaonekana.
Kwa upande wa ujenzi wa miundo mbinu na hususani
barabara, Mhe. John Malecela, amesema Serikali ya Mhe.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete inafanya kazi
kubwa na nzuri ya kuendeleza ujenzi wa
mitandao ya barabara nchi nzima.
“ Kusema ukweli, Mhe. Kikwete anajitahidi sana katika
eneo hili hakuna nchi katika eneo la Afrika
Mashariki ambayo inaweza
kushindana nasi kwa upande wa barabara.” Akasema Mhe.
Malecela
Na kuongeza serikali haijaishia katika ujenzi wa barabara
lakini pia inaendelea na jukumu uimarishaji wa reli,ujenzi na upanuzi wa
bandari ukiwamo ujenzi wa bandari mpya katika eneo la Bagamoyo. Bandari
aliyoieleza kwamba itakapokamilika
itakuwa na uwezo wa kuegesha meli kubwa na
zenye uwezo wa kubeba tani nyingi za mizigo.
Akizungumzia uzefu wake katika tasnia ya
diplomasia na ushirikiano wa
Kimataifa. Mhe, John Malecela
ambaye pia ni mwanadiplomasia mkomavu aliwataka
maafisa hao kutoyumba pale inapobidi kutetea misimamo na maslahi ya nchi yao.
“ kwa kweli ninawaonea
huruma sana Mabalozi wa wakati huu, mnafanya kazi katika mazingira magumu sana,
enzi zetu nakumbuka nikiwa hapa Umoja wa
Mataifa miaka michache baada ya kupata
uhuru Balozi ulikuwa na nguvu ya kusimama kwenye majukwaa ya kimataifa na kutetea jambo bila
ya kuwaogopa wakubwa”. Akasema.
Na kuongeza, “ Kuna mkutano mmoja nilitoa maneno makali dhidi ya Balozi wa Israel wakati ule. Baada ya
mkutano ule, Balozi yule alikuja ofisini kwangu na kuniambia maneno
yale niliyoyasema hayakuwa msimamo wa
nchi yangu”.
“ Lakini pia
niliitwa nyumbani na Baba wa
taifa, Mwalimu Nyerere. akaniambia John umezungumza nini huko, taratibu hao ni wakubwa na mimi nikamjibu, Mhe. Rais naamini nimekuwakilisha
vizuri. Ninachotaka kusisitiza ni kwamba
msiogope kutetea maslahi ya nchi yetu licha ya changamoto za diplomasia
za nyakati hizi”. Akasisitiza
1 comment:
Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
Post a Comment