Advertisements

Thursday, November 7, 2013

Madhara ya kufanyakazi na wanawake warembo-2


Zipo njia nyingi za kitaalamu za kupima ili kubaini kuwa mwanaume anakabiliwa na tatizo hili au la! Lakini pamoja nazo ni hii ya kujibu maswali, ambayo imeonekana kuwa ni rahisi zaidi kwani haihitaji mtaalamu wa kumuongoza mhusika bali ni kwa mtu mwenyewe kutafakari na kupata majibu kama urembo wa mwanamke unaweza kumuathiri kiutendaji. Maswali ya kujiuliza ni haya:

>>Je, una uwezo wa kuongea na mwanamke bila kushika shika vitu? Kwa mfano kuingiza mikono mfukoni, kuchezea simu, kalamu au hata kujipapasa mwenyewe?

>>Je, unaweza kutazamana naye usoni kwa zaidi ya sekunde 36 bila kuona aibu? Unaweza kutembea hatua nne mbele ya mwanamke bila kuhisi mwili wako ni mzito?

>>Je, unajiamini unapokuwa na mazungumzo na mwanamke hasa mkiwa wawili tu, au mpaka uwe na mtu mwingine?
>>Je, umewahi kuwa na ukaribu na wanawake warembo wangapi na kati yao ni wangapi uliwatongoza?

Baada ya kujiuliza maswali hayo sahihisha kulingana na majibu yako. Endapo utakosa yote fahamu kuwa wewe ni miongoni mwa watu wanaoweza kupata athari ukipewa nafasi ya kufanya kazi na wanawake warembo. Kumbuka kuwa jibu la mwisho lazima idadi yake isizidi nusu, endapo umewahi kuwa na urafiki wa karibu na wanawake warembo 10 kwa mfano na kati ya hao watano au zaidi uliwatongoza, utambue kuwa una viashiria vibaya vya kupata madhara tunayoyazungumza.

Ifahamike pia kwamba watu wanaotafunwa na ‘virusi’ hivyo vinavyoletwa na mvuto wa wanawake warembo ndiyo hao ambao hutumia vyeo au nafasi zao vibaya kwa kuajiri au kutoa nafasi za upendeleo kazini kwa wanawake wasiokuwa na sifa za kufanya kazi husika na hivyo kujikuta ofisi, wizara na hata biashara zinakosa tija.

Wakati nafanya uchunguzi kuhusu tatizo la kushirikiana kikazi na wanawake warembo ambapo niliwahoji baadhi ya wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara maswali niliyoandika hapo juu, wengi walibainika kuwa na tatizo hili, hata hivyo changamoto iliyokuwepo ni juu ya swali lao la msingi kwamba wafanye nini wasiathiriliwe kisaikolojia baada ya kuwepo kwa dalili za tatizo?
Jibu la swali hili ni dogo nalo ni kujitambua na kuwa makini.

Inashauriwa kuwa watu wenye matatizo haya wanatakiwa kudhibiti mawazo yao ya kimapenzi mara wakutanapo na wanawake warembo na kusimamia vitu halisi. Jambo la mwisho ni kujiamini na kutenda yale wanayofahamu.

Katika hali ya kawaida tatizo la mvuto wa wanawake hugusa zaidi hisia, hivyo mara nyingine ni vigumu kwa mtu kuweza kuzuia msukumo usitokee, lakini kwa aliyejitambua itakuwa rahisi kwake kutoendeleza mawazo ya kimapenzi sambamba na kazi.
Wakati mwingine ni suala la mtu mwenyewe kuamua kusimamia kazi na kupuuza hisia za kimapenzi zilizotokana na mvuto wa mwanamke mrembo, kwa vile si lazima kila mawazo au hisia zinazotokea ziendelezwe.

Hebu tujiulize ni mara ngapi huwa tunawaza au kuhisi vibaya na tukaacha kufanya kama tulivyofikiri kabla? Je, hakuna vipindi ambavyo huwa tunawaza kuua, kuacha wake zetu na hata kufanya mapenzi na ndugu na mambo mabaya kama hayo na tukayapuuza mawazo hayo? Ikiwa tumeshafanya hivyo tufahamu kuwa nguvu kubwa iko kwenye uamuzi wetu.

Nikimalizia somo hili ni kwamba, mara nyingi wanaume wenye aibu na hofu mbele ya wanawake ni wale wanaodhani kuwa wanakasoro fulani ambazo zinaweza kuwakosesha penzi na hivyo kuamua kujikarabati kwa unyenyekevu, sauti za chini, hongo, kutembea kwa madaha na wakati mwingine kujifanya ni watu wa tofauti sana kwenye jamii, jambo ambalo huweza kuathiri mwenendo wao na kuwa watu wa kuigiza mambo yasiyoendana na uwezo wao halisi au kile wanachokifahamu.

imalizie mada hii kwa kufafanua kuwa lengo la makala haya si kuzuia ushirika kati ya wanaume na wanawake warembo bali kufundisha watu kuhusu madhara yake ili ukiwapo urafiki uwe ni ule wenye tija, usioathiri ufanisi wa kazi.

GPL

No comments: