ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 28, 2014

MHE. MWIGULU NCHEMBA AZUNGUMUZA NA WANANCHI WA KATA YA IFAKARA

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Ifakara wakati wa Mkutano wa Kufungua Kampeni uliofanyika Jana Tar.27/02/2014.Hapa akiwa na Wahanga wa siasa chafu zinazodaiwa Kufanywa na
Chadema kupitia Vijana wake wa Redbrigade.Mwenye T-shirt ya Njano ni Mzee Alphonce John ambaye alitopolewa Macho kwa dispisi wakati wa Uchaguzi wa Udiwani huko Kahama Mwezi uliopita.
Mwigine mwenye Shati la Kijana ni Kijana Musa Tesha ambaye alimwagiwa Tindikali na Vijana wanaodaiwa Kuwa wa Chadema huko Igunga wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo.
Mh:Mwigulu Nchemba jana amesisitiza Wananchi wa Kalenga kuwa makini na siasa Chafu za Chadema zinazofanywa sehemu mbalimbali hasa kwenye nyakati kama hizi za Uchaguzi.Amesisitiza kuwa kwenye Chaguzi zozote Vyama vya siasa vinashindanisha Sera na hoja kuhusu Maendeleo ya Wananchi wa eleo hilo,Mkataba wa CCM na Wananchi ni Maendeleo katika Taifa hili,Umoja na Mshikamano ndio ngao ya MwanaCCM yeyote.
Mwigulu Nchemba amesema dhambi ya Mauaji na Unyama unaoendelea kwenye mikutano ya siasa na maeneo mbalimbali haitamwacha Dr.slaa Salama kutokana na yeye kuwa kiongozi anayebariki Siasa chafu hizo.
Chanzo:Kalenga

2 comments:

Anonymous said...

Hizi ni Siasa chafu za CCM kutembeza wagonjwa wanaodaiwa kuumizwa na CHadema ambayo sio kweli kisa kutafuta kuchukua jimbo la Kalenga huu ni uhuni r Nchemba. Tafuteni nafasi kwa ukweli wa nini mnawafanyia wananchi. Hao mtawatembeza hadi lini. Hamna la kuwaambia wananchi wanaotaabika na mali zao. Maji masafi hawana, barabara mbovu, shule na hospitali hakuna vitanda. Hii ni aibu tosha. CCM mnaimaliza Tanzania.

Anonymous said...

ccm ndo yenye siasa chafu tena wao ndo wanaofanya matukio halafu wanawasingizia wanasiana wa upinzani wadanganyika kaeni mmkijua kila mnapoichagua ccm na ndo kila mtakapo kuwa walalahoi daima.

akili ni mali tumeyeni akili zenu wadanganyika wenzangu